Frank Lampard wa Chelsea akishangilia kufunga goli la timu yake dhidi ya Stoke City kwenye Uwanja wa Britannia mjini Stoke-on-Trent, England jana Januari 12, 2013. Chelsea walishinda 4-0. |
Siku ya kufa nyani... Jon Walters alijifunga mbili na akakosa na penalti |
Walters (kulia) akijiandaa kupiga kichwa cha mkizi na kujifunga goli la kwanza |
Walters (kushoto) akijifunga la pili kwa kichwa |
Walters (19) akipaisha penalti yake mbele ya kipa wa Chelsea Petr Cech |
JON Walters alitupia magoli mawili ya kujifunga na akakokosa na penalti wakati Chelsea ilipoisambaratisha Stoke 4-0 na kumaliza mendo wao wa kuvutia wa mechi 17 nyumbani bila ya kufungwa katika Ligi Kuu ya England.
Walters aliitumbukiza wavuni mwake kwa kichwa cha mkizi krosi ya Cesar Azpilicueta muda mfupi kabla ya mapumziko na akarudia tena kufunga kwa kichwa kwenye lango lao wenyewe kufuatia kona ya Juan Mata.
Frank Lampard alifanya matokeo yawe 3-0 kwa njia ya penalti baada ya Mata kuchezewa madhambi ndani ya boksi kabla ya Eden Hazard kufunga goli kali la nne kwa shuti la umbali wa 30 akitumia mguu wa kushoto.
Siku mbaya ya Walters ilikamilika wakati alipopaisha penalti yake juu ya mwamba katika dakika za lala salama.
Mchezaji huyo raia wa Jamhuri ya Ireland mwenye umri wa miaka 29 amesifiwa sana kwa kiwango chake akiwa na Stoke msimu huu lakini mechi yake ya 100 ya Ligi Kuu ya England iligeuka kuwa shubiri.
Chelsea walikwea hadi nafasi ya tatu kwenye msimamo katika mechi walionekana kuwa na bahati lakini walisumbuliwa kwa muda mrefu na walishukuru macho sahihi ya mshika kibendera mwanadada Sian Massey kwa kukataa kihalali penalti waliyopewa Stoke wakati matokeo yakiwa 1-0.
Refa Andre Marriner aliamuru ipigwe penalti wakati Azpilicueta alipoteleza na kumuangusha Matthew Etherington ndani ya boksi, lakini Massey alikuwa tayari ameshamnyanyulia Etherington cha kuotea.
Stoke, ambao hawajawahi kuifunga Chelsea kwenye Uwanja wa Britannia, walianza mechi vizuri, wakiwashambulia wageni kwa mipira mingi ndani ndani ya boksi na wakamshuhudia Kenwyne Jones akifumua shuti pembeni kidogo ya lango.
Demba Ba alikuwa akicheza mechi yake ya kwanza ya Ligi akiwa na Chelsea lakini, katika dakika za awali, alikuwa 'bize' katika nesu yao ya uwanja na mara mbili aliokoa hatari langoni kwao.
Ba, ambaye alichezeshwa badala ya Fernando Torres mbele, alihusika katika matukio mengi katika kipindi cha pili.
Alimpasia kwa kisigino Lampard ambaye aliingia ndani ya boksi na kufumua shuti lililopanguliwa na kipa Asmir Begovic, na wakati mwingine alikimbia vyema na kumlazimisha kipa kuokoa kiufundi.
Matokeo ya mechi za jana Jumamosi Jan. 12, 2013:
- QPR 0 - 0 Tottenham
- Aston Villa 0 - 1 Southampton
- Everton 0 - 0 Swansea
- Fulham 1 - 1 Wigan
- Norwich 0 - 0 Newcastle
- Reading 3 - 2 West Brom
- Stoke 0 - 4 Chelsea
- Sunderland 3 - 0 West Ham
MSIMAMO WA LIGI kUU YA ENGLAND BAADA YA MECHI ZA JANA:
Nafasi | Timu | Mechi | Goal Difference | Pointi |
---|
1. | Man Utd | 21 | 26 | 52 | |||
2. | Man City | 21 | 22 | 45 | |||
3. | Chelsea | 21 | 24 | 41 | |||
4. | Tottenham | 22 | 12 | 40 | |||
5. | Everton | 22 | 9 | 37 | |||
6. | Arsenal | 20 | 18 | 34 | |||
7. | West Brom | 22 | 1 | 33 | |||
8. | Liverpool | 21 | 8 | 31 | |||
9. | Swansea | 22 | 5 | 30 | |||
10. | Stoke | 22 | -3 | 29 | |||
11. | West Ham | 21 | -3 | 26 | |||
12. | Norwich | 22 | -10 | 26 | |||
13. | Fulham | 22 | -5 | 25 | |||
14. | Sunderland | 22 | -5 | 25 | |||
15. | Southampton | 21 | -10 | 21 | |||
16. | Newcastle | 22 | -12 | 21 | |||
17. | Wigan | 22 | -17 | 19 | |||
18. | Aston Villa | 22 | -25 | 19 | |||
19. | Reading | 22 | -16 | 16 | |||
20. | QPR | 22 | -19 | 14 |
إرسال تعليق