
KWA
siku mbili mfululizo, jana na juzi, ujumbe kupitia njia ya simu ulikuwa
ukisambaa kwa kasi na kuvumisha kuwa mwimbaji gwiji wa miondoko ya
taarab hapa nchini, Bi Khadija Kopa, amefariki dunia.
Juzi
usiku Saluti5 ilimpigia simu Khadija Kopa baada ya uvumi huo kuzagaa,
simu yake ikapokelewa na mtu mwingine na kusema kuwa kwa muda ule Bi
Khadija tayari alikuwa ameshalala lakini mtu huyo akaithibitishia
Saluti5 kuwa habari hizo si za kweli.

Jana
jioni uvumi huo ukaibuka tena ambapo Saluti5 ilipokea simu nyingi za
wasomaji wake zilizotaka kujua ukweli juu ya jambo hilo.
Saluti5
ilipoongea na Khadija Kopa jana usiku, alisema hajui uvumi huo umetokea
wapi. “Labda kuna Khadija mwingine aliyefariki kwenye familia nyingine
ya Kopa”, alisema Bi Khadija na kuongeza kuwa pengine pia ni njia ya
watu kumtakia maisha marefu.
Chanzo:- Saluti5
إرسال تعليق