Mama akamatwa kwa kumuuza mwanawe India

Umaskini huwafanya watu wengi India kufaya vitendo kama vya kuwauza watoto
Mama mmoja Kaskazini mwa India katika jimbo la Rajasthan, amekamatwa kwa madai ya kumuuza mwanawe kwa dola 12,000.
Mama huyo alisema kuwa alimuuza bintiye ili aweze kupata pesa za kulipia faini aliyokuwa ametozwa ya dola elfu tano na baraza la kijiji.
Polisi wamemkamata mwanamume na mwanamke ambao wanadai kumnunua mtoto yule.
Umaskini na hali ngumu ya maisha huwapelekea wanawake nchini India kuwauza watoto wao, na wasichama wengi pia huuzwa.
Polisi wanasema kuwa msichana huyo aliuzwa mwezi mmoja uliopita lakini uhalifu huo ulijulikana wakati alipojaribu kuwatoroka watu waliokuwa wanamnunua mtoto huyo.
Washukiwa walimfukuza lakini wakafanikiwa kuingia katika mkahawa mmoja ambapo watu walimtambua na kuita polisi.
Msichana huyo alimbia polisi kuwa watu waliokuwa wamemnunua walimchapa na walikuwa wanapanga kumuuza kwa watu wengine mjini Mumbai.
"tulimkamata mamake msichana huyu, na wanunuzi wawili,'' alinukuliwa akisema mkuu wa kitengo cha kupambana na uuzaji haramu wa watu.
Biashara ya watoto ni mojwapo ya dhulma zinazofanyiwa watoto wa kike nchini India
Polisi wanasema kuwa imegundulika kuwa wakati wa uchunguzi, mama huyo pia alijaribu kumuoza msichana huyo kwa mwanamume kitamaduni ambapo mume anamlipa mahari mama.
Lakini baadaye alifutilia mbali makubaliano yake na mwanamume yule na kumchukua msichana wake. Na hapo ndipo baraza la wzee wa kijiji lilimtoza faini kwa kosa hilo.

Post a Comment

Previous Post Next Post