Jaribio la Nuklia Korea lazua mgogoro

Wanaharakati wapinga nguvu za nuklia Korea Kaskazini
Gazeti la taifa nchini China limeonya kuwa Beijing haitasita kukomesha msaada kwa Korea Kaskazini ikiwa itafanya jaribio lengine la kinuklia.
Taarifa kwenye gazeti hilo, Global Times, inajiri baada ya Kaorea Kaskazini kujibu vikali hatua ya kuwekewa vikwazo vikali zaidi dhidi yake na Umoja wa Mataifa mwezi jana.
China iliunga mkono viwazo hivyo, lakini gazeti hilo limesema kuwa Pyongyang haikuonekana kufurahia hatua ya China kutaka vikwazo hivyo kulegezwa.
China ni mshirika mkubwa wa Korea Kaskazini,
Pia inaarifiwa kuwa China inataka uthabiti katika rasi ya Korea lakini haitakuwa mwisho wa dunia ikiwa mgogoro mdogo utaibuka.
Korea Kaskazini imeonya vikali Korea Kusini dhidi ya kujihusisha na vikwazo hivyo vya Umoja wa Mataifa.

Post a Comment

Previous Post Next Post