Mancini kuikatia rufaa kadi nyekundu ya Kompany.

 Meneja Roberto Mancini Manchester City amekasirishwa na maamuzi ya mwamuzi Mike Dean kufuatia kumtoa uwanjani kwa kadi nyekundu ya moja kwa moja(straight red card) mlinzi wake tegemeo Vincent Kompany kufuatria kumfanyia “tackling” Jack Wilshere wa Arsenal.
Kadi hiyo itamuweka nje ya dimba kwa michezo mitatu jambo ambalo litaathiri kikosi City katika changamoto ya kuwania taji licha ya kwamba klabu imedai kuikatia rufaa.
Amenukuliwa akisema
'hii siyo kadi nyekundu kabisa, haiwezekani nimpoteze mchezaji kwa michezo mitatu bila sababu. Haikuwa faulo mimi nina umri wa miaka 48, lakini niemona vizuri sana hii ‘tackling ilikuwa ni ya kimchezo'

Post a Comment

أحدث أقدم