MBUNGE FILIKUNJOMBE ASIFU WAWEKEZAJI WA MAKAA YA MAWE NA CHUMA YA MCHUCHUMA NA LIGANGA ,AITAKA SERIKALI KUBORESHA BARABARA .....

Mbunge  wa  jimbo la Ludewa  Deo  Filikunjombe wa nne  kulia akiwa na  viongozi mbali mbali wa wilaya ya Ludewa  pamoja  na wafanyakazi wa kampuni ya kichina  iliyowekeza katika mradi  wa makaa ya mawe ya mchuchuma na liganga  Ludewa kutoka  kulia ni mke wa mbunge huyo Sarah Filikunjombe , katibu  wake Stanley Gowele, kushoto  mwenyekiti  wa CCM wilaya ya Ludewa Stanley Kolimba , katibu mwenezi wa CCM mkoa wa Njombe Honoratus Mgaya na mwakilishi wa NDC

MBUNGE wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Deo Filikunjombe ameitaka serikali kuharakisha mchakato wake wa kuboresha miundo mbinu ya barabara ya Njombe - Ludewa  kama njia ya kuharakisha uanzishwaji  wa miradi mikubwa ya makaa ya mawe na chuma ya  Mchuchuma na LIGANGA.

Filikunjombe alitoa kauli hiyo leo baada ya kutembelea kambi ya wawekezaji wa kampuni ya Tanzania China International Mineral Resouces Ltd ( TCIMR).

Pia mbunge huyo mbali ya kusifu kampuni hiyo ya kimataifa bado amepongeza kasi nzuri ya mwekezaji wa ndani wa kampuni ya M.M.I kuwa wameendelea kufanya vema na kuwa uzalendo mkubwa unaofanywa na mwekezaji huyo na hao wa kichina KATIKA mirado hiyo ni ukombozi mkubwa kwa wana Ludewa na Taifa kwa ujumla.

Alisema kuwa toka mchakato wa kuanza ndoto ya kunufaika na madini hayo kuanza kampuni hiyo ya kichini ambayo ni kampuni ya kimataifa ndio imeonyesha kasi nzuri ya uwekezaji .

Hata hivyo alisema mbali ya kampuni hiyo kuonyesha mafanikio makubwa kampuni bado changamoto kubwa ambayo inakwamisha maendeleo ya mradi huo ni serikali kuchelewa kukamilisha ahadi yake ya ujenzi wa barabara ya Njombe- Ludewa japo tayari upembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi huo umeanza.

" Nimetembelea eneo la wawekezaji Leo nimefurahishwa sana na kasi nzuri wanayokwenda nayo ila changamoto zipo ndogo ndogo Kama ya serikali kuharakisha ujenzi huo wa barabara pia kwa Upande wa wananchi wanahimizwa kulima kwa wingi mboga  mboga na kufuga nguruwe... "

Kwa Upande wake mkurugenzi mtendaji wa TCIMR Huang Daxiong alisema kuwa lengo la kampuni yake ni kuharakisha zaidi uanzwaji wa mradi huo pamoja na kuwepo kwa changamoto za kuchelewa Kutoa mizigo yao bandarini ,ufinyu wa barabara ya Njombe- Ludewa na sheria Kali za upitishaji wa mizigo Kutoka Dar es Salaam kuja eneo la mradi .

Pia alisema hadi sasa changamoto kubwa ya kiafya inayowakabili ni ugonjwa wa malaria ambao umekuwa ukiwatesa zaidi wafanyakazi wa kichina waliopo eneo hilo.

Wakati huo huo   Filikunjombe amewataka wananchi wanaozunguka  mradi wa makaa ya mawe  na mchuchuma kutokuwa na hofu juu ya lugha kwani tayari amewaagiza wawekezaji wa kichina waliopo katika mradi huo kuwa na mkalimani ambae anajua kichina na kiswahili ili kuondoa mgongano wa lugha .

Pamoja na kuwaagiza wawekezaji hao wa kichina kuwa na mkalimani bado amewataka wananchi wa jimbo hilo kusomesha watoto wao na pale inapowezekana basi kujifunza lugha ya kichina pia ili kuweze kuwasaidia wananchi wengine kutoburuzwa kwa lugha na kunufaika na raslimali za wilaya hiyo ya Ludewa.

Filikunjombe aliyasema hayo wakati akizungumza  na wananchi wa kata ya Nkomang,ombe  Mara baada ya kutembelea mradi huo ,mbunge Filikunjombe alisema kuwa wananchi hao wanapaswa kutokuwa na hofu juu ya wawekezaji wanakwenda kuwekeza wilaya ya Ludewa.

Alisema kuwa hadi  mwaka 2014 kampuni hiyo itakuwa imejenga Kiwanda katika eneo hilo na Nkomang'ombe kwa ajili ya mradi wa makaa ya mawe na mchuchuma hivyo kuwataka wananchi kuanza kuweka mazingira ya kunufaika na miradi hiyo hiyo .

Pia alisema kuwa pamoja na wananchi wa Ludewa kuanza kunufaika na matunda ya Uhuru sasa baada ya kukosa uhuru toka mwaka 1961 nchi ilipopata uhuru wake bado wananchi wanapaswa kuishi vizuri na wawekezaji wanaofika kuwekeza katika wilaya ya Ludewa yenye utajiri mkubwa hapa nchini.

Filikunjombe alisema kuwa kuanza kufanya kazi kwa miradi hiyo mikubwa kumeanza kufungua milango ya maendeleo katika wilaya ya Ludewa ambayo toka nchi ipate uhuru imekuwa nyuma kwa maendeleo.

Aidha alisema kuwa mbali ya kuwa mradi huo ulikuwepo toka nchi ikipata uhuru ila toka kipindi hicho mradi huo ulikuwa hauja weza wanufaisha wananchi wa Ludewa na kupongeza hatua iliyofikiwa kwa sasa kuwa ni nzuri na itawakomboa wananchi wa wilaya hiyo na mkoa wa Njombe pamoja na Taifa kwa ujumla.

Post a Comment

أحدث أقدم