Licha ya kufanya karakati za kutengeneza video mpya ya wimbo wake
"yatakwisha" aliyofanya na lina, ambayo mpaka hivi sasa ipo katika hatua
za mwisho, Ben pol amesema mfumo wa digital umemvunja nguvu na
kumpunguzia kasi, kwasababu kumekuwa na mvurugano kwenye televisheni
zetu na hivyo kuwa sio kipindi kizuri cha kufanya biashara, maana watu
wengi kama asilimia 85 hawana access ya kuona video kwa ufasaha, kwahiyo
anaweza akaipoteza tu video hiyo.
"nafikiri kuanzia march au april ndio nitatoa maana naamini vitu vitakua
vimenyooka, kiujumla nimepanga nitoe video mbili kwa mwaka huu, moja
nitoe mwanzoni na nyingine iwe juu ya mwezi wa sita, either wa nane au
wa tisa." amesema Ben Pol.
إرسال تعليق