Mimi Ndio Mmiliki Halisi wa Wema Sepetu" - Martin Kadinda


BAADA ya kuwepo kwa vingi viulizo juu ya Wema Sepetu na mwanamitindo Martin Kadinda kwenda Afrika Kusini wawili tu, modo huyo wa kiume amevunja ukimya na kusema kuwa, haina haja ya kushangaa kwani yeye ndiyo kila kitu kwa msanii huyo.
.
Akizungumza kwa kujiamini hivi karibuni, Kadinda alisema yeye kama meneja wa Wema, ana kila sababu ya kuongozana naye kila anapokwenda kwani ndiye anayemchagulia nguo, viatu hadi ‘setting’ ya nywele.

“Watu wamesemasema sana juu ya safari yangu ya Sauzi na Wema…jamani mimi ni kila kitu kwa Wema kwani ni meneja wake, napaswa kujua kila anachokifanya, hata linapokuja suala la mavazi mimi ndiye ninayemchagulia ‘so’ watu wasihoji sana,” alisema Kadinda.

Post a Comment

أحدث أقدم