Suleiman Kova
MSHTAKIWA wa kesi ya wizi wa Fedha katika Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), katika Benki Kuu ya Tanzania, Ajay Somani
amefariki dunia baada ya kujipiga risasi.
Habari
zilizolifikia Mwananchi Jumamosi wakati tunakwenda mitamboni na
kuthibitishwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi,
zinasema kuwa Jay alijipiga risasi jana asubuhi, maeneo ya Upanga karibu
na Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
“Alijipiga
risasi saa 2 asubuhi nyumbani kwake Upanga, karibu na Hospitali ya
Muhimbili.”, alisema Kamanda Minangi na kuongeza kuwa haijajulikana
tukio hilo kwa kwa hakuacha ujumbe wowote.
Jay alikuwa
anakabiliwa na mashtaka ya wizi wa pesa hizo kiasi cha Sh5.9, katika
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, yeye pamoja na ndugu yake Ajay Soman,
ambaye anatumikia kifungo cha miaka miwili jela baada ya kupatika na
hatia katika kesi nyingine ya EPA.
Mbali na ndugu
hao wawili, washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Kanda wa Chama cha
Mapinduzi(CCM), Rajabu Maranda na binamu yake Frijala Hussein, ambao
tayari wanatumikia kifungo gerezani baada ya kupatikana na hatia katika
kesi nyingine tatu za EPA.
Katika kesi
hiyo, washtakiwa wengine ni waliokuwa wafanyakazi wa BoT, Ester Komu,
aliyekuwa Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Madeni na Bosco Kimela aliyekuwa
Kaimu Katibu wa BoTna Imani Mwakosya, ambapo walisomewa maelezo ya awali
Julai 26, 2012 na kesi hiyo iko katika hatua ya usikilizwaji wa
mashahidi wa upande wa mashtaka.

إرسال تعليق