MBUNGE wa
Jimbo la Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo (Chadema), amerejea nchini
kutoka Uingereza alikokuwa akitibiwa na kusema sasa yuko fiti
kuwatumikia wananchi wake.
Hata hivyo
taarifa ya ujio wake ilifanywa kwa siri kiasi kwamba hata picha za
kupokewa kwake Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA)
hazikuweza kupatikana.
Mbunge huyo anarejea nchini baada ya kukaa Uingereza tangu Septemba 2012.
Taarifa hizo zilithibitishwa na katibu wake, Basil Lema ambaye pia ni Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro.
Mbunge huyo anarejea nchini baada ya kukaa Uingereza tangu Septemba 2012.
Taarifa hizo zilithibitishwa na katibu wake, Basil Lema ambaye pia ni Katibu wa Chadema Mkoa wa Kilimanjaro.
“Ni kweli
Ndesamburo amerejea Jumamosi na ndege ya Shirika la British Aiways na
alitamka mwenyewe kuwa “Nimerejea na niko fiti,”alisema Lema akimkariri
Ndesamburo.
Lema aliongeza kusema “Sasa mbunge wetu amerudi na ametangaza afya yake imetengemaa kikamilifu na yuko tayari kwa ajili ya kukuru-kakara za kuwatetea wananchi wake.”
Lema aliongeza kusema “Sasa mbunge wetu amerudi na ametangaza afya yake imetengemaa kikamilifu na yuko tayari kwa ajili ya kukuru-kakara za kuwatetea wananchi wake.”
Hata hivyo,
jitihada za kumpata Ndesamburo kwa njia ya simu yake ya kiganjani jana
zilishindikana kutokana na simu yake hiyo kuzimwa, lakini baadhi ya
ndugu wa karibu walisema yuko fiti.
Novemba
mwaka jana mwenyewe aliongea na gazeti hili na kuthibitisha kuwa anaumwa
na anapatiwa matibabu nchini humo huku akiwatoa hofu wapiga kura wake
kuwa hajazidiwa hata kidogo.
Akizungumza
kwa simu na gazeti hili juzi usiku, Ndesamburo alisema kwa sasa
anaendelea vizuri na kwamba anasubiri ruhusa ya madaktari wake ili aweze
kurejea nchini.
Post a Comment