NEWS:- WANANCHI WA DUMILA-MOROGORO WAFANYA FUJO.


Wafunga barabara kuu ya kuelekea dodoma na kufanya fujo kama inavyoonekana katika picha msururu wa magari ya abiria na mizigo yakiwa upande wa kutoka Dumila kwendaa Kilosa yakisubiri kufunguliwa kwa Barabara ya Kilosa – Dumila,Wilaya ya Kilosa, baada ya wananchi wenye
hasira kufunga njia hiyo kwa kuweka mawe makubwa na magogo ili kushinikisha kusikilizwa na kutekelezewa madai yao dhidi ya wafugaji kama yalivyokutwa Msowero

Wananchi wa Kijiji cha Mambegwa na Msowero katika Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyo, Halima Dendego ( hayupo pichani), alipozungumzanao baada ya kuziba kwa mawe makubwa na magogo Barabara ya Kilosa- Dumila eneo la Msowero,kwenye daraja la mto Msowero na kusababisha hadha ya usafiri wa magari ya abiria na mizingo, kama walivyokutwa juzi eneo hilo.
Baadhi ya wananchi pamoja na Askari wa Polisi wakipita kwa shida katika daraja la mto Msowero baada ya wananchi wenye hasira kufunga barabara ya Kilosa- Dumila, na kusababisha hadha kubwa ya magari kushindwa kupita akwa siku nzima ya kama ilivyokutwa eneo hilo.
Askari Polisi wakiwashikiria vijana waliojaribu kuleta fujo wakati wa mkutano wa Mkuu wa Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro Halima Dendego (hayupo pichani) katika Kijiji cha Msowero,baada ya wananchi wa Vijiji vya Mambegwa na Msowero kuamua kufunga Barabara ya Kilosa- Dumila kwa magogo na mawe wakishinikiza kusikilizwa madai yao ya migogoro ya mipaka ya Vijiji vya wafugaji na wakulima kama walivyokutwa eneo hilo, hata hivyo Mkuu wa Wilaya alifanikiwa kuafikiana nao na kufungua njia hiyo saa 12 jioni baada ya kuifunga saa 12 asubuhi ya siku hiyo.

Mkazi wa Kijini cha Msowero, Tarafa ya Magole, Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro, ambaye jina lake halikuweza kufahamika akibeba baiskeri yake begabi baada ya wananchi wenye hasira wa Kijiji cha Mambegwa kufunga barabara ya Kilosa- Dumila kwenye daraja la Msowero na kusababisha usumbufu na hadha kubwa ya magari kushindwa kupita kama ilivyokutwa katika eneo hilo.

Post a Comment

Previous Post Next Post