Wafunga barabara kuu ya kuelekea dodoma na kufanya fujo kama
inavyoonekana katika picha msururu wa magari ya abiria na mizigo yakiwa
upande wa kutoka Dumila kwendaa Kilosa yakisubiri kufunguliwa kwa
Barabara ya Kilosa – Dumila,Wilaya ya Kilosa, baada ya wananchi wenye
hasira kufunga njia hiyo kwa kuweka mawe makubwa na magogo ili kushinikisha kusikilizwa na kutekelezewa madai yao dhidi ya wafugaji kama yalivyokutwa Msowero
hasira kufunga njia hiyo kwa kuweka mawe makubwa na magogo ili kushinikisha kusikilizwa na kutekelezewa madai yao dhidi ya wafugaji kama yalivyokutwa Msowero
Wananchi wa Kijiji cha Mambegwa na Msowero katika Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro wakimsikiliza Mkuu wa Wilaya hiyo, Halima Dendego ( hayupo pichani), alipozungumzanao baada ya kuziba kwa mawe makubwa na magogo Barabara ya Kilosa- Dumila eneo la Msowero,kwenye daraja la mto Msowero na kusababisha hadha ya usafiri wa magari ya abiria na mizingo, kama walivyokutwa juzi eneo hilo.
Mkazi wa Kijini cha Msowero, Tarafa ya Magole, Wilaya ya Kilosa, Mkoa wa Morogoro, ambaye jina lake halikuweza kufahamika akibeba baiskeri yake begabi baada ya wananchi wenye hasira wa Kijiji cha Mambegwa kufunga barabara ya Kilosa- Dumila kwenye daraja la Msowero na kusababisha usumbufu na hadha kubwa ya magari kushindwa kupita kama ilivyokutwa katika eneo hilo.
إرسال تعليق