Meza
yetu ya habari imepokea taarifa fupi toka Mtwara usiku huu
ikitujuza kuchomwa moto kwa gari moja linalosadikiwa kutumika kwa
biashara ya abiria (TAX) huko Mtwara. Chanzo chetu kimezidi kunyetisha
kuwa mkasa huo unapewa mahusiano na sakata la GESI linaloendelea hivi
sasa hapa nchini, kwani gari hiyo inasemekana lilitaka kumtorosha Bibi
mmoja mkazi wa kijiji cha Msimbati - Mtwara aliyetoa ahadi kuwa gesi
ikisafirishwa kutoka Mtwara kwenda Dar es salaam kama serikali
ilivyokusudia basi itageuka kuwa Maji na si gesi tena! Inasemekana bibi
huyo alitaka kwenda kuonana na wazee
wa kimila na kuongea na kuhusu suala zima la gesi, bado
haijafahamika nini bibi huyo alitaka kujadili na wazee hao wa
kimila.Hadi sasa haijajulikana nani kahusika na tukio hilo na
haijajulikana kama kuna watu wameumia kutokana na tukio hilo.
Kuwa karibu nasi kwa habari zaidi .................................
Post a Comment