OMBI JINGINE HILI HAPA KWA LITAKAE MGUSA

  
Ujumbe wa kwanza hapo chini kabla ya ombi la mwenye shida ni kwa wachangia maoni ya hovyo hovyo humu ndani:

Tatizo sio kiasi gani mtu kaomba na kuwa naweza kutoa au siwezi. Na sio kweli kwamba naweza kusaidia kila kitu cha kila mtu, kwa hela ipi?

Swala hapa linakuja ni kwamba maombi ni mengi kuliko uwezo wa anaetumiwa, wanaotakiwa kushiriki kutoa misaada ni wenye moyo tu na sio comments tupu zisizo saidia chochote.
Yanayowezekana kusaidiwa yanasaidiwa, yasiowezekana yanatafutiwa njia mbadala kama hii.

Kama kuna yoyote hapendezwi na hizi post, anaweza kukaa kimya au kutafuta shughuli nyingine ya kufanya.
Sina mpango wa kufungua NGO, sababu sio kila kitu kila mtu anatakiwa kufanya.

Wenye  moyo watasaidia, na nafahamu njia hii ni rahisi na pekee ambayo naweza kutumia kufikisha ujumbe.
Na tayari wapo waliokwisha saidiwa kupitia post za humu na hawajalalamika story zao kuwekwa.

Sasa comments za hovyo hovyo vema mkazitunza au mkazitumia kwenye blogs za aina ya comments zenu, sio humu. Kwani hazita postiwa kamwe. Ni upotezefu wa muda na nguvu zenu.
Kutoa hamuwezi, mnakalia majungu na kukosoa kila kitu. mxii

Wenye moyo kuna na hili jamani.

BINTI MWANAHAWA JUMA ALLY ANAHITAJI ADA YA SHULE

Barua yake imetoka kwa mkuu wa shule

Anasoma: Kidato cha tatu
Shule: YESHUA SEC SCHOOL
S.L.P 46213
Tel: 0714 146464
Dar es salaam

Yah: Mwanahawa Juma Ally

Husika na kichwa cha habari hapo juu, mtajwa hapo juu ni mwanafunzi wetu ktk shule hii wa kidato cha tatu (3), tunatambua ana tabia njema, maendeleo yake ya masomo ni mazuri wastani, tunaomba huduma ya kulipiwa ada kwa wakati.

Ada muhula wa kwanza 250,000
Ada muhula wa pili        100,000
Ada ya mtihani mock       10,000
Tahadhari                         10,000
Michango mingine             25,000
Masomo ya ziada              10,000
Mahafali ya kidato cha nne   5,000

Jumla ya deni analodaiwa hivi sasa ni Tshs. 395,000/=

Account ya shule ni
YESHUA SEC SCHOOL - CRDB AZIKIWE - 01J024516700

Na kuna mahitaji mengine anatakiwa kuwa nayo kama madaftari, kalamu, School bag, Viatu vya ngozi pair 2, Soksi, Vifutio, Vichongeo n.k.


Asanteni.

Post a Comment

Previous Post Next Post