Kwa muda wa saa zaidi ya nne leo, wasanii kadhaa wa Bongo Flava na
wadau wa muziki walikuwa wakijadili kwenye mtandao wa Twitter tatizo
sugu la uuzwaji wa kazi zao mitaani (kuburn cd). Mjadala huo ulianzishwa
na Profesa Jay aliyeanza kwa kutweet:
Roho inaniuma sana nikiona sehemu imeandikwa, TUNABURN BONGO FLAVA
HAPA, TUNAWEKA KWENYE FLASH, KWA BLUTOOTH PIA.. Hivi kweli TUMESHINDWA??
Tweet hiyo ilivuta attention ya wasanii wengi na wadau wa muziki wakiwemo MwanaFA, Chege, Roma na Ditto:
Hivi ndivyo walivyojadili:
Hivi ndivyo walivyojadili:
MwanaFA: @Profesa_Jay ndio inavyoelekea…tumeshindwa…ishakuwa kitu cha kawaida kabisa..tutakufa hatujafaidika na huu mziki…
Profesa: @MwanaFA unadhani tukijipanga upya kwa dhati kabisa hatutafanikiwa? TUANZIE WAPI?
MwanaFA: @Profesa_Jay natamani tungekuwa hatukuwahi kujaribu,pengine
ningekuwa na moyo bado..unajua watu wetu walivyo..binafsi kama
nimechemsha hivi
Profesa: @MwanaFA sawa sawa ngoja tuone labda tutakutia tena moyo
urudi kundini maana nguvu yako na uwezo mkubwa wako ni muhimu sana kwa
hili jambo!
Roma: @MwanaFA @Profesa_Jay KULIFANYA TATIZO LIISHE KABISA NI VIGUMU LAKINI UNAWEZA KULIPUNGUZA
Profesa:@Roma_Mkatoliki @MwanaFA @Profesa_Jay na hilo ndilo
linalotakiwa haswa maana piracy ipo dunia nzima ila hapa imepitiliza!
MwanaFA: @Profesa_Jay @Roma_Mkatoliki yeah,ikipungua tu itasaidia..ipungue kwa kiwango kikubwa..kwisha kabisa haiwezekani
Ditto: @Profesa_Jay Mafanikio kwenye kukomesha hilo Upo kwenye mikono yetu wenyewe.
Roma: @Lameckditto @Profesa_Jay hivi kuna uwezekano bongo movie wana umoja sana kuliko sisi? na chama/club yao ipo active?
Chege: @Profesa_Jay hakuna kinacho shindikana chini ya jua
mwamba,huo mchakato haujatolewa macho tu na serikali yetu,inauma sana
kiukweli, eti imekua kitu cha kawaida tu ukitoa vieo mpya kesho unakuta
inauzwa ubungo mataa!
Profesa: @ChegeChigunda Jamaa wanaona kama ni haki yao ya msingi
hivi kuwanyonya wasanii we ngoja tuu SIKU ZAO ZINAHESABIKA….
NYAMBAAAAAAF
إرسال تعليق