SHANGHAI SHENHUA YAPINGA UHAMISHO WA DROGBA KWENDA GALATASARAY.


 Uhamisho wa Didier Drogba kuelekea Galatasaray ya Uturuki uko mashakani kufuatia klabu yake ya Shanghai Shenhua kusisitiza kuwa mshambuliaji huyo ana mkataba nao.
Galatasaray ilitangaza kumsaini Drogba jumatatu kwa mpango wa uhamisho wenye thamani ya euro milioni €6 mpaka kiangazi 2014.
Shenhua imesema imesema inajipanga kuweka pingamizi.
Taarifa iliyotolewa na Shenhua kupitia mtandao wa klabu hiyo ikisomeka  "Klabu imeshtushwa sana. Drogba bado ni mchezaji wa Shanghai Shenhua kwa kuwa ana mkataba nasi nab ado yuko katika kipindi halali cha mkataba.
"Shanghai Shenhua iko tayari kuepeleka ushahidi FIFA ili kupinga jaribio hilo”

Post a Comment

Previous Post Next Post