IKICHEZESHA wachezaji
wake vijana wanaoinukia vema, Simba SC jioni hii imelala 1-0 mbele ya
Black Leopard ya Afrika Kusini katika mchezo wa kirafiki uliofanyika
Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Bao pekee la washindi
katika mchezo huo, lilifungwa na beki Hassan Isihaka aliyejifunga katika
harakati za kuokoa dakika ya saba tu ya mchezo huo.
Pamoja na kufungwa,
watoto hao wa Simba SC waliokwenda ziara ya wiki mbili Oman, walicheza
soka maridadi na kuwaburudisha wapenzi wa timu hiyo.
Ushindi huo, unaitoa
mrithi Leopard ambayo awali katika ziara yake ya wiki moja nchini
ilifungwa mechi mbili na Yanga SC, 3-2 Dar es Salaam Jumamosi na 2-1
jana CCM Kirumba, Mwanza.
Katika mchezo huo,
kikosi cha Simba kilikuwa; Abuu Hashim, William Weta, Emiry Mgeta,
Hassan Isihaka, Hassan Hatibu, Said Ndemla, Ramadhani Singano, Ibrahim
Ajid/Haruna Shamte, Marid Kaheza, Rashid Ismail na Miraji Madenge.
Leopard; Azwindn
Maphala, Ermort Azaga, Thulan Ntishgila, Humphey Khoza, Vicent Mabusela,
Tiyana Mabunda, Mongezi Bobe, Mahlatse Maake, Michael Nkambula , Mxolis
Ngunede na Kodney Ramagalela
Bin Zubeiry blog.
إرسال تعليق