SIMBA SC ILIVYOUA KWA SUMU ZA OMAN LEO, HUYO NGASSA BALAA NA KASEJA BADO WAMO, KUNA CHANONGO USIMPIMIE


Mshambuliaji wa Simba SC, Mrisho Ngassa kulia akipongezwa na wenzake baada ya kufunga jioni hii katika ushindi wa 3-1 dhidi ya African Lyon katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uliofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Ngassa alifunga mabao mawili.

Ngassa akishangilia na Haruna Moshi 'Boban kwenye benchi', huku wachezaji wengine wakimtazama kwa shauku

Beki wa Simba SC, Mussa Mudde akimdhibiti mshambuliaji wa Lyon

Juma Kaseja amepangua penalti ya Shamte Ally 

Beki wa Lyon, Job Ibrahim akikimbilia mpira dhidi ya kiungo wa Simba SC, Ramadhani Chombo 'Redondo'

Job Ibrahim akijaribu kumkimbiza kiungo wa Simba SC, Amri Kiemba kulia

Job akiwa amelala kuondosha mpira miguuni mwa Ngassa

Haruna Chanongo akiruka kwanja la beki wa Lyon na kufanikiwa kupiga krosi iliyounganishwa nyavuni na Ngassa kuwa bao la tatu

Mabeki wa Lyon wakimdhibiti kiungo wa Simba SC, Amri Kiemba

Kiemba akipambana na mabeki wa Lyon 

Ngassa akimtoka Job Ibrahim kufunga bao la pili leo 

Redondo akifunga bao la kwanza

Haruna Chanongo akipasua msitu wa mabeki wa Lyon

Job akiwa amepitia mpira miguuni mwa Ngassa

Redondo akimshukuru Ngassa kwa pasi ya bao la kwanza la Simba

Mwinyi Kazimoto akichuana na kiungo wa Lyon

Kikosi cha Lyon leo
Kikosi cha Simba SC leo


Picha na Bin Zubeiry

Post a Comment

أحدث أقدم