Tahadhari kwa raia wa kigeni Libya

Ubalozi wa Marekani uliteketezwa na balozi wakekuuawa wakati wa maandamano dhidi ya nchi za magharibi
Raia wa Uingereza wametakiwa kuondoka mji wa Benghazi nchini Libya mara moja, baada ya kutokea vitisho dhidi yao.
Kwa mujibu wa maafisa wa wizara ya mambo ya nje ya Uingereza, ubalozi wa Uingereza mjini Tripoli umeweza kuwasiliana na raia wa uingereza na kwamba imepokea taarifa zao.
Ulisema kuwa hauwezi kutoa taarifa za ziada, kuhusu vitisho hivyo lakini ukasisitiza kutoa tangazo la onyo kuhusu usafiri nchi Libya.
Wizara ya mambo ya nje imekuwa ikiwashauri watu dhidi ya kusafiri kwenda Benghazi na maeneo mengine mengi ye Libya tangu mwezi Septemba.
Katika onyo lake la hivi karibuni kuhusu safari za nchini humo, wizara ya mambo ya nje imesema kuwa baada ya hatua ya jeshi la Ufaransa, kuingilia mzozo wa Mali kumekuwa na uwezekano wa mashambulizi ya kulipiza kisasi, dhidi ya maslahi ya nchi za kimagharibi katika eneo hilo.
Pia kuna uwezekano wa kufanyika visa vya utekaji nyara nchini Libya.
Tarehe 11 mwezi Septemba mwaka jana, balozi wa Marekani Chris Stevens na maafisa wengine watatu , waliuawa kwenye mashambulizi hayo dhidi ya ubalozi wa Marekani mjini Benghazi.
Balozi huyo alifariki kutokana na moshi mkubwa aliponaswa ndani, ya jengo lililokuwa linateketea baada ya watu waliokuwa wamejihami kuvamia ubalozi huo.
Bi Hillary Clinton akijitetea kuhusu mashambulizi ya Benghazi kwani wakati huo alikuwa waziri wa mambo ya nje
Bi Hillary Clinton aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wakati wa shambulizi hilo, alijitetea mbele ya kamati ya bunge kuhusu mashambulizi hayo siku ya Jumatano
Aidha Bi Clinton, alitoa ushahidi wake wakati , akihojiwa kuhusu uvamizi,huo na kusema kuwa kundi la
al-Qaeda limekuwa likieneza harakati zake katika eneo hilo.

Wiki jana, katika nchi jirani ya Algeria, wanamgambo hao waliteka kiwanda cha gesi na kuwateka nyara mamia ya wafanyakazi wa kigeni ambako wanajeshi wa Ufaransa wamekuwa wakipambana na wapiganaji hao wa kiisilamu.
Inaaminika kuwa raia 37 wa kigeni waliuawa ikiwemo raia sita wa Uingereza wakati wa siku nne za, makabiliano kati ya kikosi maalum cha wanajeshi wa wanamgambo hao.

Post a Comment

أحدث أقدم