
Carols Tevez
Mshambulizi wa Manchester City, Carlos Tevez,
amepigwa marufuku kuendesha gari kwa muda wa miezi sita ijayo, baada
ya kupatikana na hatia ya kutojibu barua zilizotumwa kwake na polisi,
kuhusiana na mashtaka ya kuendesha gari kwa mwendo wa kasi zaidi.
Tevez, 28, amekanusha madai kuwa ndiye aliyekuwa
akiliendesha gari hilo wakati, camera za polisi zilipoinasa kuwa
inakwenda kwa kasi.
Akijitetea,
Tevez alisema kuwa hakutambua barua hizo zilikuwa zikitoka kwa polisi
kwa kuwa hakufahamu maana ya nene "constabulary".
Mchezaji huyo kutoka Argentina, alikiri mashtaka mawili mbele ya hakimu mkuu mkaasi wa Manchester ya kutotoa habari kwa polisi.
Tevez pia alipigwa faini na kuamrishwa kulipa gharama za keshi ambazop kwa ujumla ni pauni elfu moja mia tano na hamsini.
Wakili wa Tevez, Gwyn Lewis, alifahamisha
mahakama hiyo kuwa mteja wake anaelewa maana neno polisi na kusema
kwamba Tevez haelewi maana ya neno gumu kama vile Constabulary.
Wakili huyo alisema barua hiyo iliandikiwa imetoka Cheshire Constabulary na kwamba hakuna neno polisi hata moja.
Machi 28 mwaka uliopita, Tevez alipatikana na
hatia ya kutotoa habari kwa polisi wakati gari lake liliponaswa
likiendeshwa klwa mwendo wa kasi.
BBC SWAHILI
إرسال تعليق