Kampuni
ya Simu ya Tigo imetambulisha huduma mpya kwa wateja ujulikanayo kama
Tigo Time , ambayo inatoa punguzo kubwa sana la gharama ya kupiga simu
saa 24/7 ikitegemeana na wakati, siku na eneo atakapo kuwa mteja husika.
Mbunifu
wa Ofa za Tigo Bi. Jacqueline Nnunduma (Pichani) amesema Tigo inatambua
kwamba wateja wake wanahitaji huduma bora na kwa gharama nafuu nah ii
ni njia moja wapo ya kuhakikisha kuwa wateja wao wanapata huduma zenye
ubora wa juu na vifurushi ambavyo vitawapatia unafuu wa bei kwa muda
wote.
Kwa
punguzo hili kubwa la bei lililopita kifani, hakuna shaka kuwa Tigo
Time itakuwa huduma maarufu kama ilivyo huduma ya ‘Kwa Sekunde’
iliyoanzishwa miaka kadhaa iliyopita.

إرسال تعليق