Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WADAU wa sanaa hapa nchini,
wameendelea kummwagia sifa mwanadada Wastara Juma, aliyekuwa mke wa
marehemu Sadiki Juma Kilowoko, maarufu kama Sajuki kuwa ana moyo wa aina
yake.
(Pichani ni Marehemu Juma Kilowoko 'Sajuki' enzi za uhai wake akiwa na mke wake kipenzi chake, Wastara).
Hiyo imetokana na historia ya
uhusiano wake na Sajuki hadi kufunga ndoa kukumbwa na mitihan mingi,
jambo ambaloh hivyo halikumfanya ajiweke kando na Sajuki.
Akizungumza katika mahojiano maalum,
Mbunge wa Kigoma Kaskazini, kwa tiketi ya Chadema, Zitto Kabwe, alisema
kwamba Wastara ana mapenzi ya dhati na anastahili sifa.
Alisema ameweza kumuuguza mumewe
mwanzo hadi mwisho wa uhai wake, jambo ambalo limekuwa gumu kwa baadhi
ya watu, kadri muda unavyozidi kwenda mbele.
"Ni mfano wa kuigwa kwakweli kutokana
na historian a matatizo mengi yaliyowakumba yeye na mumewe hadi
kufariki na kuzikwa Ijumaa katika makaburi ya Kisutu," alisema.
Naye Mbunge wa Kinondoni, kwa tiketi
ya (CCM), Idd Azzan, alisema amekuwa karibu na sanaa kiasi cha kumuona
Wastara ni miongoni mwa wanawake makini.
"Kwa dunia ya leo kumuuguza mume wako
katika kipindi kigumu cha ugonjwa wake, hadi kuchangiwa fedha za
kumpeleka India, hakika baadhi yao wanaweza kuleta wasiwasi kidogo,”
alisema Azzan.
Azzan ni miongoni mwa wabunge
wanaofuatilia sanaa kwa karibu zaidi, huku wasanii wengi wakikimbilia
kwake kila wanapokuwa na jambo linalohusu msaada kutoka kwa jamii nzima.
Post a Comment