Golikipa wa timu ya Black
Leopards,Posnett Omony akisota kuokoa mpira uliotinga wavuni kutoka kwa
mchezaji wa timu ya Yanga,Jerry Tegete kwa njia ya penati mnamo dakika
ya 54.Timu ya Yanga imeibuka kifua mbele mpaka dakika 90kwa kuinyuka
goli 2-1 timu ya Black Leopards kwenye mchezo wao wa marudiano wa
kirafiki uliofanyika kwenye uwanja wa CCM-Kirumba jijini Mwanza.Picha na
JICHIE BLOG-jijini Mwanza.
Mchezaji wa wa timu ya Yanga David
Luhende akitaka kumchomoka mchezaji wa timu ya Black Leopards,Moses
Kwena,kwenye mchezo wao wa marudio uliofanyika kwenye uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza jioni ya leo.
Wachezaji
wa timu Yanga wakifurahia goli la pili lililofungwa na Jerry Tegete
kipindi cha pili mnamo dakika ya 54 kwa njia ya penati.
Pichani ni Golikipa wa Black Leopards Posnett Omony akijitahidi
kuokoa mpira uliopigwa kwa kichwa na mchezaji wa Yanga,Said Bahanuzi na
hatimaye kutinga kimiani mnamo dakika ya saba.
Mchezaji Hamis Kiza wa Yanga akifanya jitihada za kumchomoka beki wa timu ya Black Leopards,Victor Kamhuka.
Mchezaji wa wa
timu ya Yanga David Luhende akitaka kumchomoka mchezaji wa timu ya Black
Leopards,Moses Kwena,kwenye mchezo wao wa marudio uliofanyika kwenye
uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Baadhi ya mashabiki wa Mpira wakiwa
wamepanga mstari kwa ajili ya kununu tiketi na kujionea kandanda safi
kabisa kati ya timu ya Yanga na Black Leopards ya Afrika kusini.
Kikosi cha Yanga kikiwa katika picha ya pamoja.
Sehemu ya umati wa watu waliokuwa
wakishuhudia mchezo huo,ambapo timu ya Yanga imetoka kifua mbele goli
2-1 dhidi ya timu ya Black Leopards ya Afrika Kusini,mchezo huo
umechezwa leo kwenye uwanja wa CCM-Kirumba jijini Mwanza.
Mtanange ukikaribia kuanza.
Kikosi cha timu ya Black Leopards.
Benchi la ufundi la timu ya Yanga
Ilikuwa ni patashika ngua
kuchanika,mchezaji wa timu ya Yanga,Jerry Tegete akiwatoka baadhi ya
mabeki wa timu ya Black Leopards,Jerry alifanikiwa kufunga goli la pili
mnamo dakika ya 54 kipindi cha pili.
إرسال تعليق