Wateja kupata salio mara mbili kila anapotuma pesa kupitia Airtel Money
· Ni kwa wateja wa malipo ya awali nchi nzima
kampuni ya simu za mkononi ya
Airtel leo imezindua promosheni mpaya ya Airtel Money ambapo wateja
wakel watapata muda wa maongezi mara mbili ya gharama watakazotozwa kwa
kutuma pesa na kupata wateja muda wa maongezi kulingana na ada ya
makato pale wanapotoa pesa kwa kupita huduma ya Airtel money.
Akizungumza kuhusu promosheni
hiyo, Meneja Uhusiano Jackson Mmbando alisema” Tumewawezesha wateja wetu
kutumia huduma ya Airtel money na kufanya miamala mbalimbali ya pesa
huku tukisogeza huduma za kifedha karibu na makazi na sehemu zao za
kazi , leo tunayofuraha kuwazawadia wateja wetu waliojisajili nchini
nzima muda wa maongezi mara mbili ya gharama watakazotozwa kutuma pesa
kupitia Airtel money na pia tunawapa muda wa maongezi kulingana na ada
watakayotozwa kutoa pesa pale watakapo toa pesa kupitia Airtel money.
Bonus hii ya muda wa maongezi itatumika kupiga simu Airtel kwenda
Airtel siku nzima , kwa siku nzima hadi saa sita usiku.”
“Tunaendelea kuboresha huduma yetu
ya Airtel money na kuendelea kutoa suluhisho la huduma za kifedha hasa
katika maeneo yenye changamoto ya huduma za kibenki. kwa kupitia mtandao
wetu mpana ulioenea zaidi tuna wawezesha watanzania nchni nzima hasa wa
maeneo ya vijijini kupata huduma za fedha zilizo salama , nafuu na
gharama nafuu kupitia Airtel Money.
Promosheni hii ya pata muda wa
maongezi itaondoa Kampeni ya bure, na kuanzia sasa wateja wa Airtel
watazawadia muda wa maongezi kila wanapotuma na kupokea pesa kupitia
huduma ya Airtel Money”. Aliongeza Mmbando.
Airtel bado inaendelea kutoa
huduma za mawasiliano za simu zenye ubora na gharama nafuu , kwa sasa
wateja wa Airtel wa malipo ya Awali wanatuma ujumbe mfupi was ms kwa
shilingi moja mara baada ya kutuma ujumbe mfupi wa kwanza kwa shilingi
125na kupiga simu kwa senti 10 mara baada ya dakika mbili za mwanzo.

إرسال تعليق