
Muuza matunda mmoja nchini India aliyekuwa amehukumiwa adhabu ya kifo
tangu mwaka 2001 kwa kosa la kupanga kufanya shambulizi katika bunge la
nchi hiyo amenyongwa. Maafisa wamesema Mohammed Afzal Guru aliyekuwa
akisubiri adhabu hiyo tangu 2002 amenyongwa katika gereza la Tihar
karibu na Delhi.
Afzal Guru amekuwa akikana kuhusika na shambulizi hilo lililosababisha
vifo vya watu tisa. India imeimarisha ulinzi na kutangaza amri ya
kutotembea hovyo katika Jimbo la Kashmir ambako taarifa za kunyongwa
huko zingeweza kuzua vurugu. India ni nadra sana kutekeleza adhabu za
kunyongwa ambapo Afzal Guru anakuwa mtu wa pili tangu mwaka 2004, baada
ya Mohammed Ajmal Kasab.
Post a Comment