Polisi
wakiwa wameimarisha ulinzi nje ya jengo la Sukari lililopo mkabala na
Makutano ya Barabara za Ohio na Sokoine Driver Posta jijini Dar es
salaam jengo hilo ndmo zilimo ofisi za mwendesha mashtaka wa Serikal
Dk.Eliezer Feleshi,
Ulinzi huo umeimarishwa kutokana na tishio la wafuasi wa Shekh Ponda
kutishia kuandamana kwenda kwa Mwendesha Mashtaka huyokushinikiza Shekh
Ponda aachiwe huru.
Baadhi
ya wafuasi hao wa Shekh Ponda wamekamatwa katika maeneo mbalimbali
wakati wakijaribu kuingia katika eneo la Posta ambapo ulinzi mkali
uliimarishwa huku polisi wakitumia Magari, Pikipiki, Mbwahuku makachero
wakizunguka kila mahali.
Baadhi
ya Barabara zilifungwa ili kuweka eneo hilo katika hali ya usalama
zaidi na kuhakikisha linzdhibitiwa na kulidwa kirahisi.
Poalisi wakiimarisha Doria katika maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.
Askari
Polisi wakifanya doria kwa kutumia pikipiki kam wanavyoonekana
wakiranda katika mitaa mbalimbali Posta jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wafuasi wa Shekh Ponda wakiwa wamekamatwa kwa tuhuma za kufanya maadamano bila kibali cha polisi.
Wafuasi hao wa Shekh Ponda wakipandishwa kwenye gari la polisi mara baada ya kukamatwa katika maandamano hayo.
Zoezi la kuwakamata na kuwapeleka polisi watuhumiwa hao likiendelea chini ya ulinzi mkali.
Magari mbalimbali yakiwa yamebeba askari Polisi yakipita mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es salaam.
Polisi wa Pikipiki wakiwa kazini leo.
إرسال تعليق