Baadhi ya wanafuzi wajiuwa kwa kufeli kidato cha nne

Habari utakayoisoma hapo chini inasikitisha na kuhuzunisha.

Imani yangu ni kuwa tunao ndugu, jamaa na marafiki ambao wamepata matokeo mabaya kwenye mitihani yao. Hivyo ninasihi tusiwe wepesi kusema, “ni shauri lake! Wacha afe! hana faida kwanza” na maneno yanayofanana na hayo, tafadhali tujiepushe na kauli hizo. 

Ikiwa unaona utashindwa kujizuia, tafadhali jitengee mazingira ya kutokuonana kwa muda mrefu na mhusika, hadi hapo hasira zako zitakapotulia uweze kuzungumza naye ukiwa na “sound mind” kwa kuwa hasira huleta hasara zaidi -- two wrongs won't change the situation, nor make it right.

Wahudumu wa Afya, tuwe msitari wa mbele kutoa ushauri na nasaha, “counselling” tunapoweza na kwa tunavyoweza.

This isn’t a joke. It’s shockingly very bad and sad!
Matokeo mabovu kuliko yote ya Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha Nne kuwahi kutokea katika historia ya taifa la Tanzania yamezua balaa la aina yake baada ya wanafunzi wawili kujiua kwa kujipiga vitanzi hadi kufa.

Taarifa zilizothibitishwa leo na jeshi la Polisi zimeeleza kuwa wanafunzi waliojiua kutokana na matokeo hayo ni wa jijini Dar es Salaam na mwingine kutoka mkoa wa Tabora.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Anthony Rutta, amesema leo kuwa mhitimu aliyejiua mkoani humo ni Michael Fidelis (19) mkazi wa Mtaa wa Mwinyi, Kata ya Chemichemi aliyemaliza katika Shule ya Sekondari ya Kanyenye mjini Tabora.

Kamanda Rutta amesema kuwa Fidelis amejiua kwa kujinyonga hadi kufa baada ya kwenda kuangalia matokeo juzi Jumatatu (Februari 18, 2012), saa 11:00 jioni. Baadaye akakutwa amejinyonga chumbani kwake kwa kutumia kamba ya manila, kisa ikiwa ni kupada divisheni ziro.

Sehemu ya ujumbe alioacha marehemu Fidelis ulisomeka hivi: “Nisamehe sana mama, usitafute mchawi... nakupenda sana. Uamuzi niliouchukua ni sababu ya matokeo mabaya, nakutakia maisha mema.”

Matokeo ya shule ya Kanyenye yanaonyesha kuwa wahitimu 85 walipata sifuri na hakuna aliyefaulu kwa daraja la kwanza wala la pili.

Jijini Dar es Salaam, aliyejiua kwa kujipiga kitanzi baada ya kufeli ni aliyekuwa mwanafunzi wa Shule ya Sekondari Debrabant iliyopo Mbagala, wilayani Temeke, Barnabas Venant (18).

Kamanda wa Engelbert Kiondo wa mkoa wa kipolisi Temeke, amesema leo kuwa Vicent alikuwa akiishi Nzasa na amejinyonga kwa manila akiwa ndani ya stoo ya nyumba yao juzi saa 10:00 jioni baada ya kuambulia daraja la nne (Div IV), kinyume kabisa na matarajio yake.

Post a Comment

Previous Post Next Post