Chidi Beenz Kuachia Track Nyingine Hivi Karibuni.

 
Rapper Kutoka Ilala, Rashid Makwiro a.k.a Chidi Beenz anataraji kuachia mdundo wake mwingine hivi karibuni. Chidi ambae alitamba na sana ngoma zake kama Ngoma Itambae [Dar Es salaam Stand Up], Mmenisoma, Mashaalah, Nipokee na zinginezo anataraji kuachia track hiyo ambayo amefanya na mwimbaji kutoka Tanzania House Of Talent [T.H.T], nikimzungumzia Barnaba.
Chidi aliandika, "Soon nitaachia wimbo wangu mpya nimefanya na young broda Barnaba toka ThT pamooja na sauti mbili tatu za hapa na pale kutoka kwenye nyumba ile. Mwisho"
Wow!! inaonekana Chidi alipata muda wa kutosha kutembelea nyumba ile [THT]... Haha
 
King Kong ambae pia ni kiongozi wa kundi la LA FAMILIA lenye maskani yake kitaa cha Ilala, ni mmoja wa wasanii wa muziki aliyefanya collabo nyingi sana na wasanii wa kizazi kipya ikiwa ni pamoja na wasanii wa taarabu na genre nyinginezo hapa nchini.
Well... tusubirie featuring hii na Barnaba ambayo mimi pia naisubiria kwa hamu sana... One!

Post a Comment

أحدث أقدم