Dar es Salaam, Tanzania - Februari 4, 2013- Ecobank Tanzania ambayo ni
mojawapo ya benki katika kundi la Ecobank Africa iliyo katika nchi 33
Africa, inazidi kukuza uwezo wa wanabiashara Tanzania katika kushiriki
biashara kati ya Tanzania na China kwa kupunguza garama za uendeshaji
biashara kati ya nchi hizi.
Wakishiriki katika sherehe ya mwaka mpya ya China Jumapili hii katika
viwanja vya Mnazi Mmoja, Ecobank ilionyesha nia yake ya kusaidia jamii
ya waendesha biashara kati ya Tanzania na China zikiwepo huduma
zinazorahisisha wafanyabiashara wa Tanzania na wawekezaji wa Kichina
kushiriki katika uagizaji na mauzo ya nje kati ya nchi hizi. "Sisi
tunayo nia ya kutoa huduma za garama nafuu na kurahisisha upatikanaji wa
bidhaa hizi kuwezesha sekta hii inayokua kwa kasi sana.
Katika mwongo uliopita kumekuwa na uwekezaji wa $ 868 bilioni wa china
ndani ya Tanzania, huduma zetu zinajaza pengo la kurahisisha biashara
hii "anasema Bw Enoch Osei-Safo, Mkurugenzi Mtendaji Ecobank Tanzania.
Ecobank inazindua huduma ya kubadilisha hela ya Tanzania kupata sarafu
za kichina (RMB) moja kwa moja, ambapo hapo awali hapa Tanzania,
wanabiashara walilazimika kubadili TZS kwa Dola za kimarekani ili
kununua RMB. Katika mfumo huo wa awali, wanabiashara walipoteza kiasi
kikubwa cha mtaji lakini sasa, Ecobank itatwawezesha wanabiashara
kupunguza garama hizi kwa kueneza huduma hii hapa Tanzania.
" Sisi hatuwezi kupuuza matokeo ya biashara ya China juu ya Afrika,
ambayo inafikia zaidi ya dola bilioni 200 katika mwaka 2012 kwa uagizaji
na 5% ya mauzo yote ya Afrika kwenda nchini China, ushirikishwaji wa
kifedha kukuza sekta hii ni muhimu, na ndiyo maana Ecobank Group
imeonyesha nia ya kurahisisha uendeshaji wa biashara hii na kuwezesha
Afrika kuwa na ushindani na nchi zingine duniani.” Enoch aliongeza.
Ecobank Tanzania katika miezi michache ijayo itakua kituo cha kutoa
huduma za uendeshaji biashara kati ya Tanzania na China kwa kutoa huduma
ya ubadilishaji wa sarafu ya kichina na pia kulipia kodi ya forodhani
kwa TRA papo kwa papo kupitia huduma ya Asybank katika matawi yote ya
Ecobank.
Post a Comment