HZB: Majina yako kamili unaitwa nani?
KALA: Kala Jeremiah Masanja.
HZB: Kwa nini umeamua kutumia jina lako kamili na siyo nick name?
KALA:
Ujue me nimetokea bongo star seach na kule ulikua unaandikisha majina
yote kamili sasa watu kuwabadilishia jina tena naona kama na
wachanganya.
HZB: Nini maana ya 044
KALA: Ni saa kumi na dakika arobaini na nne (04:44).
HZB:Ilitokea nini 04:44?
KALA: Hahaha ilitokea nini? watu wakitaka kujua hii 04:44 wanunue album yangu nimeelezea .
HZB: Ni shule gani ambazo umepita?
KALA:
shule ya msingi nimesoma shule kama mbili hivi tofauti, Kinango pamoja
na Mendo, secondary nimesoma Donbosco,.baada ya hapo nikaingia kwenye
game ya music.
HZB: Umeanza game rasm lini? Na ngoma ipi?
KALA:
Nilianza tangu mwaka 2004, nikatoa ngoma moja inaitwa Dunia ya matangazo
nilifanyia studo za Mwanza. Kasha 2006 nikaingia bongo star seach.
HZB: Kipindi unakua ulijua kama utafanya music?
KALA:Hapana
sikujua kabisa kama ntafanya music yaani sikujua kabisa kama ntakuwa
mwana mziki mi nimeanza tu kujisitukia mwenyewe mwaka 2004 nimeanza
kupenda muziki ndo nikaandika vesi langu sasa.
HZB: Nani ambaye alikushawishi kufanya muziki kwa kipindi hicho?
KALA:Wako
wengi tu sana wan je wa bongo, ila wa bongo nilikua na album nyingi
tu kama nne nilikua na album ya Jay moo ya kwanza, nilikua na album ya
Prof jay ya kwanza nilikua na album ya Waswahili ya kwanza, na nilikua
na album ya mwana FA. Lakini album ya waswahili nilikua nasikiliza sana
hata ngoma zangu za mwanzo nimefanya kama wale jamaa,waliimbaga pengo
yupi bora kati ya rafiki, yani vile walivyokuwa wanasimamia mada
wanaichambua mada nilikua napenda sana.
HZB: Ni mafanikio gani umeyapata tangu uanze game hii ya muziki?
KALA:aaaah
mafanikio kwenye muziki yapo mengi ingawa mengine siyo ya moja kwa
moja, unajua kupitia muziki nimejulikana na kujulikana kumenisaidia meni
nimepata vitu vingi sana tofauti na muziki,naheshimiwa na watu
mbalimbali kama wazee, watoto, vijana.na wakati mwingine mzee akikuona
ankuita anakua anakuelezea matatizo yake ili niyafikishe kwa jamii, soo
nafarijika sana.
HZB:Ulisha wahi kukutana na mzee alfu akaimba hata mistari miwili katika moja ya ngoma zako?
KALA:
Yaaaa wapo wengi tu sana ujue me muziki ninao fanya unakubalika na watu
wengi,na hata ushari mwingi nachukua kwa wazee coz wao wanajua vitu
vingii sana kwa hii nchi.
HZB:Mashabiki wako unawahaidi nini kwa mwaka huu wa 2013?
KALA:
Watarajie vitu vingi tu sana kama wanavyojua Kala ni mtu wa jamii so
navitu vingi sana kwa ajili yao, ninaproject za kijamii nataka kuzifanya
mwaka huu,nitafanya mengi sana ya kijamii kwa ajili ya maendeleo ya
kitaifa na familia.
Wa mwisho kushoto ni Mama ake mkubwa, anaefuata Mama mzazi na Bibi |
HZB: Wasanii wengi kwa sasa wamekuwa wakitoa single tu na siyo album, je unahisi album hazilipi?
KALA:aaa
muziki sasa hivi umeamia kwenye show, ujue digitali kama digitali yaani
teknolojia imeleta hasara nyingi lakini pia imeleta faida nyingi, ujue
sasahivi flash nyingi, memory card nyingi, sasa mtu anawekewa tu nyimbo
hata yale mauzo ya album inakua siyo sana kama zamani, unajua sisi
zamani kama nilivyokuambia nilikua na album nne kwahiyo ulikua kupata
album kama ya Prof jay lazima unanunua tape zile bamboo ya kuban haya
kuwepo.
HZB: Kama album hailipi mbona wewe tayari umeachia album.
KALA:Hizo
ni ndoto zangu kama msanii nilikua nazo toka zamani nije kufanya album
ili mashabiki wangu ambao wanapenda kupata nyimbo zangu zote wasipate
tabu.wakati nilikua natengeneza album sikufikiria sana pesa nilifikiria
mashabiki wangu coz wengine walikua wananisikiliza kwenye radio tu
hwanielewi, soo kupitia hii album nahisi nitaongeza mashabiki.
album ya Kala |
HZB: East Africa ni msanii gani unatamani kufanyanae kazi?
KALA: Aaah wengi sana bro nikiwataja tutajaza ukurasa acha niseme wengi tu, wote wanaofanya vizuri.
HZB: Ni producer gani unamkubali hapa bongo?
KALA:
Mimi sina producer ambaye nimemkalili producer yeyote tu nafanyanae
kazi, hata album yangu ukiangalia kila wimbo unaproducer wake,unaona
kama dia God nimefanya na producer D classic ambaye alikua bado
hajajulikana lakini goma ndo kama hilo unalisikia.
D Classic |
HZB:Tukirudi nyuma kidogo ni haso gani umepitia kufanya ngoma yako ya kwanza?
KALA:Wimbo
wangu wa kwanza haukunipa tabu sana kurecord coz nilitumia bit ya mtu
niliipenda nikamwambia naomba nitumia bit yako, nikaenda studio nilikua
nimefanya mazoez na nilikua najua hakunaga kukosea, ukikosea umeharibu
wimbo mzima, soo nikafanya mazoez ya kutosha na siku naingiza mpaka Yule
producer akashangaa na likua narecord kwa lengo la kusikiliza mimi wala
sikua nafikiria kufanya muziki lakini watu walivyokua wanasikiliza
wakawa wananishawishi.
HZB: Ni ngoma gani katika ngoma zako unaikubali?
KALA:
aah ninazo nyingi sana za Kala jeremiah?.. nina red to die, ningekuwa
rais, wizi mtupu yaani magoma hayo nikiyasikia nawehuka kabisaa.
HZB: Ushauri wako kwa wasanii wanao anza muziki?
KALA:
Ushauri wangu kwanza wajiamini, pia waangalie kitu ambacho wanaiba yaani
maada inabidi watufute mada nzuri ndo itakayo wafikisha mbali, kama
kuchana kuna watu wanachana ile mbayaa.
HZB: Neno la mwisho kwa mashabiki wako?
KALA:Mashabiki wangu nawapenda sana coz bila wao mimi nisinge kuwa Kala Jeremiah unaemfahamu wewe,
UNAWEZA KUSIKILIZA MAZUNGUMZO HAPO CHINI.
إرسال تعليق