MAUAJI ya Padri wa Kanisa Katoliki Zanzibar, Evarist Mushi yaliyotokea
juzi (Jumapili) wakati akiingia kanisani kuendesha ibada ya asubuhi,
yamezua utata na inadaiwa kuna mambo mengi yaliyojificha nyuma ya
pazia.
Mauaji hayo yalifanyika kimafia katika Kanisa Katoliki, Kigangwe cha
Mtoni saa 12:45 asubuhi wakati akijiandaa kwenda kuongoza ibada
kanisani humo.
Kwa mujibu wa ofisa mmoja wa polisi, katika eneo la tukio walifanikiwa kukuta maganda mawili ya risasi na hakukuwa na wizi wowote uliofanyika baada ya padri huyo kupigwa risasi mbili kichwani.
Kwa mujibu wa ofisa mmoja wa polisi, katika eneo la tukio walifanikiwa kukuta maganda mawili ya risasi na hakukuwa na wizi wowote uliofanyika baada ya padri huyo kupigwa risasi mbili kichwani.
Mashuhuda waliozungumza na gazeti hili kwa nyakati tofauti walisema
sababu zilizofanya padri wa awali, Ambrose Mkenda apigwe risasi siku ya
mkesha wa Krismasi, mwaka jana ndizo zilizofanya na huyu auawe.
“Polisi wanaweza kujua zaidi kwa sababu tunadhani wanaendelea na uchunguzi kuhusu kupigwa risasi kwa padri Mkenda, watakuwa na fununu za kinachosababisha viongozi wa dini kushambuliwa,” kilisema chanzo chetu cha habari visiwani Zanzibar.

Hata hivyo, kuna wengine walikwenda mbali zaidi na kudai kuwa sababu za
kupigwa risasi kwa viongozi hao wa kiroho ni itikadi za kidini ambazo
uhasama wake unaongezeka kila kukicha hapa nchini.
“Ipo haja kwa serikali kuangalia hili kwani sisi watu wa dini nyingine hapa mjini (Zanzibar) tunaishi kwa wasiwasi,” alisema muumini mmoja wa Kanisa Katoliki.
“Ipo haja kwa serikali kuangalia hili kwani sisi watu wa dini nyingine hapa mjini (Zanzibar) tunaishi kwa wasiwasi,” alisema muumini mmoja wa Kanisa Katoliki.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, ACP Aziz Mohamed
alipopigiwa simu alisema atafutwe msaidizi wake ambaye hakupatikana kwa
simu.
(Picha Zote na Martin Kabemba, Zanzibar)
Post a Comment