Wanaume nao wanaweza kunyonyesha watoto wao

Unaingia katika nyumba ya rafiki yako Jumanne Mwesiga na macho yako yanakutana ana kwa ana na Mwesiga akimnyonyesha mtoto wake mchanga mwenye umri wa miezi miwili.
Utafanya nini? Kipi kitaingia katika kichwa chako kwa haraka?
Hapana shaka kuwa hili ni jambo la kushangaza kwani imezoeleka kuwa kunyonyesha ni kazi ya mwanamke.
Hata hivyo, wanasayansi kwa kutumia vigezo vya kibaiolojia wamethibitisha kuwa mwanamume anaweza kunyonyesha kama mwanamke.
Kimaumbile, mwanamume ana matiti yenye chuchu kama alivyo mwanamke. Tofauti ni kuwa matiti ya mwanamume hayana ukubwa kama yale ya mwanamke. Lakini hiyo si sababu kuwa wanaume hawawezi kunyonyesha.
Daktari wa magonjwa wa Hospitali ya Mwananyamala, John Semkuya anasema mwanamume anaweza kutoa majimaji lakini si maziwa yafaayo kwa mtoto kunyonya kama chakula chenye afya.
Anafafanuakuwai tofauti ya unyonyeshaji iliyopo kati ya mwanamke na mwanamume ni kwamba mwanamke ana tezi maalumu kichwani (pituitary glands) ambayo huzalisha maziwa
“Mwanamke yeyote ana tezi hii. Tezi hii ndiyo inayomfanya atoe maziwa na ndiyo maana zamani watoto wachanga waliofiwa na mama zao, walinyonyeshwa na bibi zao au mama zao wakubwa kwa sababu wana tezi hii,” anasema.
Dk Semkuya anasema hata kama mwanamke hajawahi kunyonyesha, kwa kawaida anaweza kutengeneza maziwa iwapo mtoto atanyonya kwa muda mrefu.
“Wapo wanaume ambao wanachezea chuchu kwa muda mrefu na kwa kufanya hivi wanaweza kusababisha maziwa kutoka,” anasema.
Kinadharia, matiti ya mwanamume kama yalivyo ya mwanamke yana tishu kama walizonazo viumbe wengine wanaonyonyesha katika kundi la mamalia ambazo ni pamoja na homoni za oxitoksini na prolactini ambazo husaidia kuzalisha maziwa.
Hata hivyo, Dk Semkuya anasema hata kama mwanamume atatoa maziwa, hayawezi kuwa na ubora kama yale anayotoa mwanamke.
- Mwananchi

Post a Comment

Previous Post Next Post