Unaingia katika nyumba ya rafiki yako Jumanne Mwesiga na macho
yako yanakutana ana kwa ana na Mwesiga akimnyonyesha mtoto wake mchanga
mwenye umri wa miezi miwili.
Utafanya nini? Kipi kitaingia katika kichwa chako kwa haraka?
Hapana shaka kuwa hili ni jambo la kushangaza kwani imezoeleka kuwa kunyonyesha ni kazi ya mwanamke.
Hata hivyo, wanasayansi kwa kutumia vigezo vya kibaiolojia wamethibitisha kuwa mwanamume anaweza kunyonyesha kama mwanamke.
Kimaumbile, mwanamume ana matiti yenye chuchu kama
alivyo mwanamke. Tofauti ni kuwa matiti ya mwanamume hayana ukubwa kama
yale ya mwanamke. Lakini hiyo si sababu kuwa wanaume hawawezi
kunyonyesha.
Daktari wa magonjwa wa Hospitali ya Mwananyamala,
John Semkuya anasema mwanamume anaweza kutoa majimaji lakini si maziwa
yafaayo kwa mtoto kunyonya kama chakula chenye afya.
Anafafanuakuwai tofauti ya unyonyeshaji iliyopo
kati ya mwanamke na mwanamume ni kwamba mwanamke ana tezi maalumu
kichwani (pituitary glands) ambayo huzalisha maziwa
“Mwanamke yeyote ana tezi hii. Tezi hii ndiyo
inayomfanya atoe maziwa na ndiyo maana zamani watoto wachanga waliofiwa
na mama zao, walinyonyeshwa na bibi zao au mama zao wakubwa kwa sababu
wana tezi hii,” anasema.
Dk Semkuya anasema hata kama mwanamke hajawahi
kunyonyesha, kwa kawaida anaweza kutengeneza maziwa iwapo mtoto
atanyonya kwa muda mrefu.
“Wapo wanaume ambao wanachezea chuchu kwa muda mrefu na kwa kufanya hivi wanaweza kusababisha maziwa kutoka,” anasema.
Kinadharia, matiti ya mwanamume kama yalivyo ya
mwanamke yana tishu kama walizonazo viumbe wengine wanaonyonyesha katika
kundi la mamalia ambazo ni pamoja na homoni za oxitoksini na prolactini
ambazo husaidia kuzalisha maziwa.
Hata hivyo, Dk Semkuya anasema hata kama mwanamume atatoa maziwa, hayawezi kuwa na ubora kama yale anayotoa mwanamke.
- Mwananchi
- Mwananchi

إرسال تعليق