Wiki iliyopita tuliona wakati ugonjwa wa Ukimwi ukiwa
haufahamiki chanzo chake, wataalamu wengi wa afya walikuwa wakihangaika
kufanya utafiti.
Tukaona wanasayansi wawili, Dk Paul Volberding na
Dk Marcus Conant walifanikiwa kubaini uhusiano kati ya ugonjwa huo na
aina ya saratani ya ngozi iliyokuwa ikiwapata wazee.
Waliweza kuihitimisha kwa kusema kuwa ugonjwa huo
unatokana na virusi hasa ukizingatia kuwa dalili ya saratani hiyo
iliyokuwa inawaandama wazee tu wakati huo ilihamia kwa vijana.
Saratani hiyo ya ngozi kwa wazee ikijulikana kama
KS wao walichokifanya ni kuuita ugonjwa huo ambao bado ulikuwa hauna
jina, KSOI.
KSOI wakiwa na maana ya ugonjwa unaowezesha mtu kufikia hatua ya kuwa na saratani ya KS.
Kwa kutamka tu kwamba ugonjwa huo unatokana na
virusi mwaka 1981, wanasayansi hao walitoa mchango wao katika mikakati
ya kuuchunguza zaidi.
Katika historia hiyo, leo tutajikita katika
kueleza wanasayansi walioipambazua dunia kwa kuweka wazi namna virusi
hao wanavyosababisha Ukimwi.
Sayansi na ugunduzi huo ndiyo uliotoa mwanya wa
kutengeneza Dawa za Kufubaza virusi hao wa Ukimwi (ARV) za kuaminika
miaka ya 1990.
Wagunduzi wa VVU
Mwanasayansi wa kwanza kutangaza kuwa ameweza kuviona Virusi Vya Ukimwi (VVU) ni Mtaalamu wa Kifaransa, Dk Luc Montagnier.
Mtaalamu huyo ambaye aliongoza jopo la wanasayansi
wengine katika taasisi ya Pasteur ya mjini Paris alitoa ripoti yake
katika jarida la sayansi mwaka 1983.
Katika utafiti huo alihusisha virusi hao na uvimbe
wa kwenye mashavu unaosababishwa na mafindofindo ambayo yalikuwa
yanawaandama sana wagonjwa wa Ukimwi.

إرسال تعليق