HII NDO "EMAIL" YA KAMANDA SULEIMAN KOVA KWA AJILI YA KUMTUMIA TAARIFA ZA UHALIFU



KAMANDA wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Suleiman Kova ametoa anwani yake ya barua pepe kwa ajili ya Watanzania waliopo ndani na nje ya nchi kusaidia kutoa taarifa za siri za kufanikisha kukamata wahalifu.

Anwani hiyo ni: kova.suleiman@yahoo.com

Kova ametaka kuwasilishiwa kwa taarifa mbalimbali juu ya vitendo vya uhalifu kupitia anuani hiyo ili kukabiliana na hujuma na tishio la usalama wa viongozi wa dini au siasa.

Alisema kutokana na vitisho dhidi ya viongozi wa dini, kushambuliwa na kuuawa Polisi imeweka mtandao utakaoshirikiana kwa karibu na viongozi wa ngazi mbalimbali ili kuhakikisha kwamba maisha, mali pamoja na taasisi zao zinakuwa katika hali ya usalama.


Chanzo: wavuti

Post a Comment

أحدث أقدم