JK AONGOZA MATEMBEZI YA MSHIKAMANO KUADHIMISHA MIAKA 36 YA CCM MJINI KIGOMA LEO

Mwenyekiti wa  Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo na Bibi Koku ambaye aliwahi kuwa Katibu wa CCM katika Wilaya mbalimbali nchini ikiwapo Dodoma, Kongwa na Mwisho Wilaya ya Kasulu wakati wa Mfumo wa Chama Kimoja.
Mwenyekiti wa  Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete leo amewaongoza maelfu ya wakazi wa Mji wa Kigoma na Vitongoji vyake katika matembezi ya Mshikamano kuadhimisha Miaka 36 ya CCM.

Rais Kikwete aliyeambatana na Mkewe Mama Salma Kikwete alianza matembezi hayo saa moja na nusu abuhi katika eneo la Mnarani Jirani na Ofisi za mkuu wa mkoa hadi CCM Mkoa wa Kigoma na kutembea kwa umbali wa takribani kilometa 5.

Wanachi na wanachama na wapenzi wa CCM walijitokeza kwa wingi katika matembezi hayo ambayo baade leo jioni Mwenyekiti huyo wa chama Taifa atahutubia mkutano wa hadhara katika Viwanja vuya Lake Tanganyika.
 

Mwenyekiti wa  Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akianzisha rasmi matembezi hayo ya Mshikamano.
 Matembezi yakiendelea
 Brass Band ikiongoza matembezi hayo.
 Viongozi mbalimbali wakishiriki matembezi hayo.

 Mwenyekiti wa  Chama cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete akisalimia wananchi marabaada ya kumaliza matembezi hayo.
 
 JK akiwapungua mkono wakazi wa Kigoma
 Viongozi wa juu wa UVCCM Taifa, Sadifa Abdallah na Mboni Mhita (kulia)
 Mkazi huyu alitoka barabarani na Binti yake
 Ulinzi ulikuwepo wakutosha

 Wananchi waliojitokeza katika matembezi hayo.
 
Mke wa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi ambaye pia ni Mjumbe wa NEC Wilaya ya Lindi Mjini akisalimia wakazi wa mjini Kigoma baada ya kushiriki matembezi.
 CCM Oyeeeeeeeeeeeeeeeh!!!!

Post a Comment

أحدث أقدم