Aidha Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete akifungua semina ya siku mbili ya Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM mjini Dodoma jana Februari 10,2013, ameponda makada wa chama hicho ambao wamekuwa wakipanda jukwaani kuhubiri kuwa ajira ni tatizo pasipo kupendekeza suluhisho la tatizo hilo.
Rais Kikwete
alisema kusimama jukwaani na kusema kwamba ajira ni tatizo hakuna maana ikiwa
mhusika hatoi pendekezo la jinsi ya kumaliza tatizo hilo.
Suala la
ajira nchini ni moja ya mada zinazotarajiwa kuwasilishwa kisha kujadiliwa
katika semina hiyo ya CCM, na Rais Kikwete aliwataka wajumbe kupendekeza jinsi
ya kuongeza ajira nchini wakati mjadala husika utakapowadia.
Hata hivyo,
Rais Kikwete alisema hivi sasa ajira katika sekta ya umma ni kama hakuna, kwani
zimebaki sekta za afya na elimu na kwamba hivi sasa suluhu ni kukuza sekta
binafsi ili kuongeza ajira.
Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi taifa (CCM)
itajulikana Jumanne, Feb. 12, mwaka huu, kisha kufanya kazi ya kuteua Kamati ya
Maadili ya chama hicho.
Kupatikana
kwa wajumbe hao kutatokana na kikao cha Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha
Mapinduzi (NEC) ambayo itakutana Feb. 11 mwaka huu, chini ya Mwenyekiti wa
chama hicho, Rais Jakaya Kikwete na kufanya uchaguzi huo.



Post a Comment