Kanisa Katoliki nchini Ujerumani limeamua kuwa ni halali kwa mwanamke kutumia tembe ya kuzuia mimba mara tu baada ya kubakwa.
Uamuzi
huu umefanywa kufuatia mkutano wa viongozi wa Kanisa Katoliki nchini
Ujerumani baada ya mwanamke mmoja aliyekuwa amebakwa kusema kuwa
alizuiwa kufanyiwa matibabu siku mbili mfululizo katika Hospitali
zinazofadhiliwa na Kanisa Katoloki zikisema kuwa kuzima mimba ni kinyume
cha maongozi yake.
Post a Comment