Wakati Kenya ilipofanya uchaguzi wake mkuu mwaka 2007, upenyezaji kwenye
intaneti katika nchi ulikuwa chini sana. Lakini leo hii, shukrani kwa
kebo za 'fibre optic' na kuongezeka kwa upatikanaji wa simu, Wakenya
wengi wanaendesha blogi na wanatumia kikamilifu akaunti za habari za
kijamii kama vile Twitter na Facebook.
Ingawaje hotuba za chuki za kisiasa zimepungua katika vyombo vikuu vya
habari, matumizi ya kauli za kuangamiza kisiasa na uchochezi vinatia
hofu kwenye kuongezeka kwake katika vyombo vya habari vya kijamii,
Ombara aliiambia Sabahi.
Vurugu za baada ya uchaguzi wa 2007-2008, ujumbe wa maandishi kwenye
simu za mkononi ulitumwa kukusanya watu na kushawishi umma, alisema.
Vurugu hizo zilisababisha kama watu 1,200 kufa na kama 300,000 kupoteza
makaazi, kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa.
Kwa kuwa na maendeleo ya teknolijia ya hivi sasa na kuongezeka kwa
vyombo vya habari vya kijamii, ujumbe wa kushawishi utaweza kuwafikia
watu maelfu na kufanya maovu makubwa zaidi.
Ombara alisema NSCMM, katika jitihada zake za kuepuka kurudia vurugu,
imeajiri wataalamu kufuatilia shughuli za vyombo vya habari vya kijamii
kukamata wakosaji ambao wanaeneza hotuba za chuki za kisiasa. Wataalamu
hawa kwa sasa wanachunguza wenye blogi watatu na kupanga gharama za
majalada dhidi yao kwa ushawishi wa kisiasa.
Sheria ya 2008 ya Tume ya Taifa ya Ushirikiano na Mshikamano inaeleza
kwamba watu wanaweza kushtakiwa kwa hotuba za chuki kama watatumia
"hotuba ambazo zinahamasisha au kuhimiza vitendo vya vurugu dhidi ya
kundi maalumu, na kuleta hali ya chuki au kutunga habari zisizo za kweli
ambazo matokeo yake yanaweza kuiweka tume kwenye uhalifu wa chuki".
Udhibiti wa 'kauli za hatari' kwenye mtandao
Mradi wa Umati, uanzishaji unaoendeshwa na kituo cha iHub cha ubunifu wa
teknolojia kilichopo Nairobi, unatumia wafuatiliaji wataalamu na
teknolojia ya kisasa kutafuta "kauli za hatari" katika vyombo vya habari
vya kijamii.
"Mradi wetu wa shirika unajaribu kufuatilia na kuripoti, kwa mara ya
kwanza, jukumu linalofanywa na vyombo vipya vya habari kuhusu uchaguzi
wa Kenya," iHub ilisema ilipotoa matokeo ya Oktoba 2012. "Mradi wetu
utakuwa na raia katika kiini chake na kutumia teknolojia husika
kukusanya, kupanga, kuchambua na kusambaza taarifa ambazo tunapokea."
Mradi wa Umati unalenga "kauli za chuki", ambazo ulizielezwa kidogo tu
kama kauli za chuki zenye uwezekano wa kusababisha vurugu. Hatimaye
mradi unatarajia kuweka ufafanuzi wa kauli za chuki ambazo zinaweza
kujumuishwa kwenye katiba.
Meneja utafiti wa iHub Agnes Crandall alisema mradi, ulifanywa kwa
ushirikiano na waandaaji wa mifumo ya kompyuta wa Ushahidi, kuajiri watu
watano wakiwakilisha makundi ya makabila makubwa matano nchini Kenya
ili kufuatilia mitandao, blogu, vyombo vya habari vya kijamii na
majukwaa mengine katika mtandao na kuripoti kauli za hatari kwa viongozi
husika.
Crandall alisema taarifa zinazotolewa zinaandikwa kwenye ripoti
inayoshirikishwa na wakala wa serikali na wabia wa vyama vya kiraia.
"Tunatoa ripoti kwa polisi, Wizara ya Habari, Tume ya Taifa ya
Mshikamano na Ushirikiano, na Tume Huru ya Mipaka na Uchaguzi,"
aliiambia Sabahi. "Kazi yetu ni kuonyesha hali ya hatari."
Katika hotuba yake ya awali ya Oktoba 2012, Umati iligundua kwamba kauli
za chuki zilizo nyingi zinatokana na watangazaji wa matukio
wasiojulikana, ikimaanisha kwamba watumiaji wanatoa majina yao halisi au
majina bandia yanayotambulika katika mitandao yao.
"Kutokuwa na hadhari wakati wa kuongea kwenye mtandao kunaonyesha kwamba
waongeaji hawazingatii athari mbaya zinazoletwa na kauli zao, wala
hawaogopi kuhusu kuhusishwa na kauli za hatari wanazozitoa," ripoti hiyo
ilisema.
Wiki iliyopita, serikali iliufunga ukurasa wa mtandao wa Mashada baada
ya Umati kugundua ukurasa huo unatumika kusambaza kauli za chuki.
Pamoja na shughuli za ufuatiliaji, wanablogu wa iHub pia wanahusisha
umma na ujumbe unaolenga kupunguza makali ya maoni ya kukasirisha
yanayotolewa kwenye mtandao, Crandall alisema.
Kuzuia uhuru wa kujieleza
Ingawa ni muhimu kufuatilia na kukomesha wale wenye uwezo wa kuiingiza
nchi katika mzunguko mwingine wa vurugu, Ndung'u Wainaina, mkurugenzi
mtendaji wa Kituo cha Kimataifa cha Sera na Mgogoro, alisema kupunguza
tamko la chuki hakupaswi kuingilia haki za kikatiba.
"Tunapaswa kuwa makini kutopunguza uhuru wa kujieleza," aliiambia
Sabahi. "[Ufuatiliaji] haupaswi kutumika kama kusingizio cha kutishia
hoja za ukosoaji za serikali au uanzishaji." Alisema utafiti wa mwisho
unapaswa kufanyika kabla washukiwa hawajapelekwa mahakamani au kufungwa
kwa tovuti kwa tamko la chuki.
Hata hivyo, Ombara, mkurugenzi wa NSCMM, aliondoa woga kwamba kufuatilia
shughuli zinazofanyika katika mtandao kutaingilia haki za Wakenya.
"Katika kila tunachokifanya, tunafuata sheria," alisema. "Ambacho
hatukipendi ni hali ambayo baadhi ya watu wanafurahia uhuru wao kwa
kutumia haki za wengine."
Vyombo vya habari vya kijamii ni upanga wenye makali pande mbili
Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Bitange Ndemo alisema inawezekana
kutumia vyombo vya habari vya kijamii kushinda uchaguzi kwa amani mwaka
huu.
"Teknolojia, hususan vyombo vya habari vya kijamii, mara nyingi ni
upanga wenye makali pande mbili," Ndemo aliiambia Sabahi. "Vinaweza
kutumika kwa kutolea ujumbe ama chanya au hasi. Ni juu yetu kuhakikisha
kwamba tunawajibika kutumia teknolojia kuboresha maendeleo yetu."
Ndemo alisema Wakenya wanapaswa kutumia njia ya mtandao kuwasiliana na
viongozi wao na kuwabana kuwajibika kwa ahadi zao, na sio kuchochea
hisia zao za kikabila na kisiasa ambazo zinaweza kusababisha vurugu.
Ili kuimarisha amani, aliwaagiza watu binafsi na mashirika kutumia
vyombo vya habari vya kijamii kuwaripoti wanaochochea chuki ili
kuisaidia serikali kuchukua hatua zinazotakiwa.
Alphonce Juma, mwenye umri wa miaka 27 anayeendesha tovuti ya "my
Aspirant my Leader", alisema teknolojia inapaswa kutumika kuuwezesha
umma.
"Badala ya kutuma au kuanzisha tovuti ambayo inawachimba Wakenya dhidi
ya wenzao, niliamua kuanzisha tovuti ambayo inawaeleza Wakenya kwamba
wanataka kujua kuhusu watu wanaogombea nafasi za kisiasa, hivyo wanaweza
kuwahusisha na hatimaye kufanya uamuzi wanaouelewa katika sanduku la
kura," alisema. "Hivi ndivyo teknolojia inapaswa kuwa."
Juma alisema tovuti yake inatoa shauku ya kisiasa na njia ya kujieleza
wao wenyewe wanapoufahamisha umma kuhusu historia za wagombea, motisha
wa kufanya kazi serikalini na mifumo ya kisiasa.
"Ninafanya hili kwa mapenzi yangu kwa sababu ninaridhika na kujisikia
kwamba ninaisaidia nchi yangu kusonga mbele," alisema. "Jitihada hizi,
kama zitafanyika kwa kila mmoja wetu katika mtandao, itasaidia kuweka
mzunguko wa vurugu za kisiasa kabatini."
Via sabahionline.com
Via sabahionline.com

Post a Comment