MTANGAZAJI ANAYETESA KENYA KWA VIPINDI VYA TAARAB - LADY F:

Fathiya Omar akiwa na Mzee Yussuf
MMOJA kati ya watangazaji wanaotesa sana nchini Kenya kwa uendeshaji mahiri wa vipindi vya taarab, ni Fathiya Omar maarufu kama Lady F anayekitumikia kituo cha PWANI FM kilichoko chini ya shiraka la utangaziji nchini humo KBC.
Kila inapotimu saa 6 hadi saa 8 mchana kila siku za Jumatatu hadi Alhamisi, maskio yote popote pale kinaposikika kituo hicho huelekezwa kwa Fathiya kupitia kipindi chake cha “Kwa raha zangu” ambapo utaburudishwa na nyimbo mchanganyiko za miondoko ya taarab pamoja na kujuzwa hili na lile kuhusiana na muziki huo.
Fathiya kama walivyo watangazaji wengine wa Kenya, aliiambia Saluti5 kuwa Taarab ya Tanzania ndiyo inayotawala zaidi nchini humo.
Historia ya utangazaji ya Fathiya, mzaliwa wa Mombasa, inaanzia Radio Salaam na baadae akajiunga na Radio Africa kabla ya kujiunga na Pwani FM ambako sasa anatimiza miaka miwili tangu aanze kukiendesha kipindi cha “Kwa raha zetu”.

Post a Comment

Previous Post Next Post