![]() |
| Fathiya Omar akiwa na Mzee Yussuf |
MMOJA
kati ya watangazaji wanaotesa sana nchini Kenya kwa uendeshaji mahiri
wa vipindi vya taarab, ni Fathiya Omar maarufu kama Lady F
anayekitumikia kituo cha PWANI FM kilichoko chini ya shiraka la
utangaziji nchini humo KBC.
Kila
inapotimu saa 6 hadi saa 8 mchana kila siku za Jumatatu hadi Alhamisi,
maskio yote popote pale kinaposikika kituo hicho huelekezwa kwa Fathiya
kupitia kipindi chake cha “Kwa raha zangu” ambapo utaburudishwa na
nyimbo mchanganyiko za miondoko ya taarab pamoja na kujuzwa hili na lile
kuhusiana na muziki huo.
Fathiya
kama walivyo watangazaji wengine wa Kenya, aliiambia Saluti5 kuwa
Taarab ya Tanzania ndiyo inayotawala zaidi nchini humo.
Historia
ya utangazaji ya Fathiya, mzaliwa wa Mombasa, inaanzia Radio Salaam na
baadae akajiunga na Radio Africa kabla ya kujiunga na Pwani FM ambako
sasa anatimiza miaka miwili tangu aanze kukiendesha kipindi cha “Kwa
raha zetu”.

إرسال تعليق