Jamal Malinzi chali kushoto Nyamlani kicheko kulia
Athumani Nyamlani (wa pili kulia)
Michael Wambura
Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Kagera na katibu mkuu wa zamani wa
klabu ya Yanga, Jamal Malinzi ameambiwa kuwa hana uzoefu wa uongozi na
hivyo kuondolewa katika kinyang'anyiro cha kuwania urais wa Shirikisho
la Soka Tanzania (TFF).
Taarifa iliyotolewa na TFF leo, imesema kuwa mgombea wa nafasi ya urais
aliyepitishwa na hivyo kubaki katika mbio za kuwania kumrithi rais wa
sasa, Leodger Tenga ni Athumani Nyamlani ambaye pingamizi alilowekewa
limetupwa baada ya kuonekana kuwa utumishi wake serikalini haumzuii hata
chembe kuongoza chombo hicho cha juu cha kusimamia mchezo wa soka
nchini. Nyamlani ni makamu wa rais wa TFF anayemaliza muda wake.
Uamuzi wa kumuengua Malinzi umetolewa leo
na Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya shirikisho hilo iliyokuwa ikipitia
pingamizi mbalimbali ambapo wengine waliongeuliwa ni katibu mkuu wa
zamani wa Chama cha Soka Tanzania (FAT- sasa TFF), Michael Wambura
ambaye alikuwa akiwania nafasi ya Makamu wa Rais na Ahmed Yahya
aliyekuwa akiwania nafasi ya uenyekiti wa Bodi ya Ligi.
Malinzi aliwekewa pingamizi na baadaye kukatiwa rufaa na Agape Fue,
aliyesema kuwa hana uzoefu.Uchaguzi wa TFF utafanyika Februari 24 mwaka
huu.

Post a Comment