TUSIFICHE UKWELI.... HIKI NDIO CHANZO CHA MAPIGANO YA JANA BAINA YA WAKRISTO NA WAISLAMU HUKO GEITA (MASLAHI YA KIUCHUMI)

Na:- Kabuga Kanyegeri
Pamoja na kuhusishwa na imani, suala hilo pia limekuwa likitazamwa kwa mtazamo wa kiuchumi hasa kwa kuzingatia kuwa hiyo ni sehemu ya ajira kwa watu wanaohusika na shughuli ya uchinjaji kwa hiyo upo uwezekano mkubwa wa hilo kuchangia katika sintofahamu hii inayoendelea.

Kwa mujibu wa duru za ndani ya kanisa hoja hiyo iliibuka katika kikao cha wachungaji Jumamosi wiki iliyopita jijini Mwanza ambako inaelezwa kuwa mtoa hoja mmoja alisema kuwa suala hilo limekuwa likiwanufaisha waislam kiuchumi wakati wamekuwa mstari wa mbele kuutukana na kuikashafu imani ya kikristo.

“Iliibuka hoja humo kwamba kila ng’ombe anayefugwa na mkristo anamuhakikishia muislamu shilingi elfu tano wakati wa kuchinja na katika hizo, shilingi elfu moja inachangwa msikitini na kwamba pamoja na yote hayo imani ya kikristo imekuwa ikikashfiwa bila serikali kufanya kitu, mtoa mada akasisistiza kuwa kuendelea kuchinjiwa na waislamu ni kuendelea kufadhili kukashifiwa kwa imani yao na kwa kuwa serikali imechukua upande katika hili ni bora wajisimamie,” kilieleza chanzo hicho.

Mwenyekiti wa Chama cha Wenye Mabucha Mwanza Machage anasema kuwa zamani kuchinjiwa ilikuwa ni kama huduma na ilikuwa ni bure pengine ndiyo maana hakukuwa na kelele za namna hii lakini sasa hivi imekuwa ni biashara.

“Chama changu, kwa mfano, tunalipa karibu shilingi milioni moja au zaidi kwa mwezi kwa ajili ya kuchinjiwa, sasa hii ni biashara kubwa ndiyo maana hata serikali inatakiwa kuliangaliwa kwa umakini mkubwa suala hili si kulichukua juu juu tu kama inavyofanya, kwa sababu yakiingia masuala ya kibiashara inakuwa si haki kusema wengine wana haki na wengine hawana haki” alisema.

HUKO KWENGINE WANAZUNGUKA MBUYU TU

Post a Comment

Previous Post Next Post