Pamoja na kuhusishwa na imani, suala hilo pia limekuwa likitazamwa kwa
mtazamo wa kiuchumi hasa kwa kuzingatia kuwa hiyo ni sehemu ya ajira kwa
watu wanaohusika na shughuli ya uchinjaji kwa hiyo upo uwezekano mkubwa
wa hilo kuchangia katika sintofahamu hii inayoendelea.
Kwa
mujibu wa duru za ndani ya kanisa hoja hiyo iliibuka katika kikao cha
wachungaji Jumamosi wiki iliyopita jijini Mwanza ambako inaelezwa kuwa
mtoa hoja mmoja alisema kuwa suala hilo limekuwa likiwanufaisha waislam
kiuchumi wakati wamekuwa mstari wa mbele kuutukana na kuikashafu imani
ya kikristo.
“Iliibuka hoja
humo kwamba kila ng’ombe anayefugwa na mkristo anamuhakikishia muislamu
shilingi elfu tano wakati wa kuchinja na katika hizo, shilingi elfu moja
inachangwa msikitini na kwamba pamoja na yote hayo imani ya kikristo
imekuwa ikikashfiwa bila serikali kufanya kitu, mtoa mada akasisistiza
kuwa kuendelea kuchinjiwa na waislamu ni kuendelea kufadhili kukashifiwa
kwa imani yao na kwa kuwa serikali imechukua upande katika hili ni bora
wajisimamie,” kilieleza chanzo hicho.
Mwenyekiti wa Chama cha
Wenye Mabucha Mwanza Machage anasema kuwa zamani kuchinjiwa ilikuwa ni
kama huduma na ilikuwa ni bure pengine ndiyo maana hakukuwa na kelele za
namna hii lakini sasa hivi imekuwa ni biashara.
“Chama changu,
kwa mfano, tunalipa karibu shilingi milioni moja au zaidi kwa mwezi kwa
ajili ya kuchinjiwa, sasa hii ni biashara kubwa ndiyo maana hata
serikali inatakiwa kuliangaliwa kwa umakini mkubwa suala hili si
kulichukua juu juu tu kama inavyofanya, kwa sababu yakiingia masuala ya
kibiashara inakuwa si haki kusema wengine wana haki na wengine hawana
haki” alisema.
HUKO KWENGINE WANAZUNGUKA MBUYU TU
إرسال تعليق