Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
Na Victor Melkizedeck Abuso
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali hatua ya serikali
ya Korea Kaskazini kufanya jaribio la tatu la zana zake za Nyuklia.
Marekani ambayo ni mwanachama wa Baraza hilo inataka serikali ya
Pyongyang kuwekewa vikwazo zaidi kutokana na jaribio hilo ambalo
wanasema limevunja maazimio la Baraza hilo yanayozuia serikali hiyo
kufanya jaribio lolote.
China ambayo ni mshirika wa karibu wa Korea Kaskazini pia imeungana na
mataifa mengine kulaani kitendo hicho na kumhoji Balozi wake mjini
Beijing kutoa maelezo ya kina kuhusu uamuazi wa serikali yake kutekeleza
jaribio hilo.
Urusi kupitai Balozi wake katika Baraza hilo la Umoja wa Mataifa Sergei
Lavrov amesema hatua hiyo ya Pyongyang inaonesha namna gani inavyopuuza
maazimio ya baraza hilo .
Mataifa kama Japan, Korea Kusini na China sasa yanahofia usalama wa watu
wake kutokana na majaribio ya mara kwa mara ya Korea Kaskazini na wiki
iliyopita Korea Kusini ilikuwa imeonesha hofu kuwa Korea Kaskzini
ingejaribu zana zake.
Tayari Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon ameshtumu hatua hiyo
anayosema imevunja azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa
kufanya jaribio hilo.
Korea Kaskazini awali ilifanya majaribio ya zana zake mwaka 2006, 2009
na mwezi Januari ilitangaza kuwa itafanya majaribio yake wakati wowote
licha ya onyo kutoka kwa Umoja wa Mataifa.
Jaribio la Korea Kaskazini limezua hali ya wasiwasi katika mataifa
jirani kama Japan na Korea Kusini huku viongozi wanaohusika na usalama
wakikutana kujadili tahadhari inayoweza kuchukua.

إرسال تعليق