Lucci leo kuachia ‘Waters up’ aliowashirikisha Julio na Jokate Mwegelo

IMG_3828 (640x427)

Producer mahiri wa nchini Tanzania Lucci, kesho anatarajia kuachia single yake mpya aliyoipa jina ‘Waters Up’. Katika ngoma hiyo aliyoiproduce mwenyewe katika studio yake iitwayo Transformax, Jokate Mwegelo na mwakilishi wa mwaka jana wa Tanzania katika shindano la Big Brother Africa, Julio wameshirikishwa.
Katika maelezo aliyoitumia Hisia za Mwananchi. Lucci amesema:
Tulirekodi mwaka jana November lakini biti niliigonga 2011. Video is coming soon. Tunatafuta mtu wa kufanya video kwa international standards kama vile jinsi wimbo ulivyo simama. Utaachiwa exclusively on Clouds Fm kwenye XXL na B12.
Namshukuru Mungu sana kwa kunipitisha katika vikwazo vingi ambaavyo vimenifanya kuwa bora na bora zaidi kama producer na msanii. Shout Out kwa my team kwa kusimama nami na kunipa support. Hupenda kutanguliza shukrani kwa Watanzania pia kwa support kwani tunawahitaji sana ili tuweze kufika mbali kimuziki katika soko la nyumbani na la kimataifa.

Post a Comment

أحدث أقدم