Ma mia ya wananchi wajitokeza nchini Tunsia kumzika kiongozi wa upinzani Chokri Belaid

Tunisians carry the coffin of Chokri Belaid during his funeral procession in Tunis
Mazishi ya kiongozi wa upinzani Chokri Belaïd, tarehe 8 Februari 2013
Na Ali Bilali

Halaiki ya watu wamejitokeza jijini Tunisia kuhudhiria mazishi ya kiongozi mkuu wa upinzani Chokri Belaid alieuawa juzi akiwa nje kidogo ya nyumbani kwake jijini Tunis.

Shughuli za usafiri wa ndege zimesitishwa, huku kukiwa hakuna usafiri kama ilivyo kawaidfa kufuatia mgomo uliotishwa na chama kikuu cha wafanyakazi nchini humo.

Ma mia ya watu wamejitokeza kuhudhuria mazishi ya kiongozi huyo aliauawa wakati alipokuwa akitoka nyumbani kwake na kukutana na mtu ambae alimlenga na kumpiga risase tatu kifuani na kufariki papo hapo, hali ambayo ilizua hasira na ghadhabu miongoni mwa wananchi waliteremka barabarani wakiandamana na wengine wakiteketeza makao makuu ya chama tawala cha Ennahda.

Wananchi waliokuw amwenye msafara kuelekea kwenye safari ya mwisho ya kiongozi huyo wa upinzani walionekana wenye huzuni na hasira huku wakitowa maneno ya kukiashifu chama tawala, huku wakimtuhumu kiongozi mkuu wa chama madarakani Ghannouchi kuwa ni muuaji, na wengine wakidai kuwa wanancbi wanahitaji mabadiliko.

Wengi wa walioshindikisha jeneza la Chokri Belaid wamesema kusikithwa na kifo cha kiongozi huyo ambae wamesema alikuw amtetezi wa wanyonge aliauwa kwa sababu alikuwa kaitetea watu masikini. Mama mmoja alisikika akisema huku akilia kwamba watu kutoka vyama tofauti ambao wanashiriki mazishi ya kiongozi huyo ni watu ambao wanataka kuw ana fikra huru kama alvyo kuwa Chokri

Wanasiasa kadhaa wa upinzani wameshiriki katika mazishi hayo akiwemo Beji Caïd Essebsi aliewahi kuwa wakati mmoja waziri mkuu katika kipindi cha mpito ambapo mshirika wake wa karibu Tatouine aliuawa mwezi Octoba mwaka jana.

Wengi ya wanasias walioshiriki katika mazishi hayo walionekana kulindwa zaidi, baada ya kupokea vitisho na vitimbi, hivyo serikali kuamuwa kuwalindia usalama zaidi na hata njia walizotumia katika kuelekea mazijkoni hazikuwekwa wazi

Post a Comment

Previous Post Next Post