![]() |
| Mazishi ya kiongozi wa upinzani Chokri Belaïd, tarehe 8 Februari 2013 |
Na Ali Bilali
Halaiki ya watu wamejitokeza jijini Tunisia kuhudhiria mazishi ya
kiongozi mkuu wa upinzani Chokri Belaid alieuawa juzi akiwa nje kidogo
ya nyumbani kwake jijini Tunis.
Shughuli za usafiri wa ndege zimesitishwa, huku kukiwa hakuna usafiri
kama ilivyo kawaidfa kufuatia mgomo uliotishwa na chama kikuu cha
wafanyakazi nchini humo.
Ma mia ya watu wamejitokeza kuhudhuria mazishi ya kiongozi huyo aliauawa
wakati alipokuwa akitoka nyumbani kwake na kukutana na mtu ambae
alimlenga na kumpiga risase tatu kifuani na kufariki papo hapo, hali
ambayo ilizua hasira na ghadhabu miongoni mwa wananchi waliteremka
barabarani wakiandamana na wengine wakiteketeza makao makuu ya chama
tawala cha Ennahda.
Wananchi waliokuw amwenye msafara kuelekea kwenye safari ya mwisho ya
kiongozi huyo wa upinzani walionekana wenye huzuni na hasira huku
wakitowa maneno ya kukiashifu chama tawala, huku wakimtuhumu kiongozi
mkuu wa chama madarakani Ghannouchi kuwa ni muuaji, na wengine wakidai
kuwa wanancbi wanahitaji mabadiliko.
Wengi wa walioshindikisha jeneza la Chokri Belaid wamesema kusikithwa na
kifo cha kiongozi huyo ambae wamesema alikuw amtetezi wa wanyonge
aliauwa kwa sababu alikuwa kaitetea watu masikini. Mama mmoja alisikika
akisema huku akilia kwamba watu kutoka vyama tofauti ambao wanashiriki
mazishi ya kiongozi huyo ni watu ambao wanataka kuw ana fikra huru kama
alvyo kuwa Chokri
Wanasiasa kadhaa wa upinzani wameshiriki katika mazishi hayo akiwemo
Beji Caïd Essebsi aliewahi kuwa wakati mmoja waziri mkuu katika kipindi
cha mpito ambapo mshirika wake wa karibu Tatouine aliuawa mwezi Octoba
mwaka jana.
Wengi ya wanasias walioshiriki katika mazishi hayo walionekana kulindwa
zaidi, baada ya kupokea vitisho na vitimbi, hivyo serikali kuamuwa
kuwalindia usalama zaidi na hata njia walizotumia katika kuelekea
mazijkoni hazikuwekwa wazi
Via kiswahili.rfi.fr

إرسال تعليق