![]() |
| Keshi |
KOCHA
Mkuu wa Nigeria, Stephen Keshi ametoa sababu za uwezekano wa kuachia
ngazi Super Eagles baada ya Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka huu,
kwamba hakubaliki nyumbani licha ya kazi nzuri anayoifanya.
‘Big Boss huyo’ aliushitua ulimwengu wa soka Jumanne kwa kusema kwenye Mkutano na Waandishi wa Habari kwamba, anaweza kuachia ngazi.
“Haijalishi kabisa watu wanafikiria nini kuhusu Stephen Keshi anachokifanya. Kitu muhimu zaidi ni ninachokifanya hapa na mafanikio ya timu yangu. Kama nikirejea nyumbani katika nchi yangu, hawaheshimu ninachokifanya katika timu, acha iwe hivyo,” Keshi alifafanua.
Iliripotiwa kwa mapana marefu kwamba, Keshi alitofautiana na viongzoi wa juu wa Shirikisho la Soka Nigeria (NFF) kufuatia Super Eagles kutoa sare ya 1-1 na Burkina Faso katika mchezo wa ufunguzi.
Keshi pia alisema kwamba hapotezi chochote kuchukiwa na viongzi wa NFF.
“Huwezi kumlazimisha mtu kukupenda wewe. Huwezi kumlazimisha mtu kukubali wewe. Itakuja yenyewe,” alisema.
Baada ya miaka 10 ya kazi ya ukocha, akiziongoza kwa mafanikio Togo na Mali, Keshi alisema anaweza kuacha kazi katika timu yake ya sasa, Nigeria baada ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2013.
“Sisi wote ni wataalamu. Kama Mungu akiniwezesha (kutwaa taji la Afcon na Nigeria leo), mapema siku ifuatayo, naweza kupakia mizigo yangu na kwenda nchi nyingine.
“Ni sawa tu na anavyofanya (Jose) Mourinho na makocha wengine wakubwa duniani. Naweza kubaki na naweza kuondoka, itategemea na mazingira.
“Mimi ni mtaalamu na tutaona itakavyokuwa. Hapa ndipo ulipo moyo wangu , nimekuwa Nahodha wa Super Eagles kwa miaka 14. Nilikuwa hapa kama kocha Msaidizi. Nipo hapa kwa sasa, lakini baada ya mashindano, tutaangalia kama kuna ofa nyingine yoyote nje ya hapa,” alimalizia.

©

إرسال تعليق