STARS, CAMEROON WAINGIZA MIL 148/-


Pambano la kirafiki la kimataifa kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Cameroon (Indomitable Lions) lililochezwa jana (Februari 6 mwaka huu) na wenyeji Stars kuibuka na ushindi wa bao 1-0 limeingiza sh. 148,144,000. 
Fedha hizo zimepatikana kutokana na watazamaji 23,092 waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa kiingilio cha sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 20,000 na sh. 30,000. 
Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama ifuatavyo; asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) ni sh. 22,598,237.29, maandalizi ya mchezo sh. 58,000,000 wakati wa gharama za uchapaji tiketi ni sh. 7,340,900. 
Nyingine ni bonasi kwa wachezaji wa Taifa Stars sh. 18,831,864.41, asilimia 20 ya gharama za mchezo sh. 8,274,659.66, asilimia 15 ya uwanja sh. 6,205,994.75 na asilimia 5 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) sh. 2,068,664.92. 
Asilimia 60 ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) sh. 24,823,978.98 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 1,241,199 ambayo ni asilimia 5 kutoka kwenye mgawo wa TFF.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Post a Comment

Previous Post Next Post